SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ishara 4 Za Upungufu Wa Maji Katika Ngozi
Urembo

Ishara 4 Za Upungufu Wa Maji Katika Ngozi 

Kuna tofauti ya ngozi iliyokosa maji ( Upungufu wa maji) na ngozi kavu, Ngozi iliyokosa maji ni ile ambayo imesababishwa na mambo ya nje kama unhealthy diet na life style choices kama unywaji wa pombe na kahawa mara kwa mara, yote haya husababisha kupunguza maji kwenye ngozi yako na kuipa ngozi muonekano hafifu lakini kwa bahati nzuri hii inaweza kutibika au kupungua endapo utabadilisha mwenendo wa matumizi ya baadhi ya vitu.

Ngozi kavu hii hutokana na asili ambapo inaweza kuwa umerithi au kuzaliwa nayo, hii haiwezi kubadilika ila unaweza ku-improve kwa kutumia bidhaa zinazoendana na ngozi yako.

Mambo 3 Ya Kuepuka Kama Una Ngozi Kavu

Ishara Za Kuwa na Upungufu Wa Maji Katika Ngozi

  • Ngozi Kuwasha

Ngozi inapokuwa kavu ina jivuta na hii husababisha miwasho, inawezekana ikawa kila mara baada ya matembezi, jua kali au upepo unafanya ngozi yako iwashe basi jua hii hutokana na kupungua kwa maji katika ngozi.

  • Kuongezeka Kuwa Sensitive

Ishara kubwa ya ngozi yako kuhitaji maji ni kuwa sensitive, na hii hutokana na kwamba vizuizi vya unyevu vimepungua kwahio ulindaji wa ngozi yako kutokana na madhara ya nje yamepungua. Bakteria na uchafu wa kawaida unaweza kuingia katika ngozi yako kwa urahisi na kusababisha ngozi ibadilike na kuwa sensitive zaidi.

  • Ngozi Kuwa Na Muonekano Dhaifu

Kama ngozi yako inaonekana kuwa dhaifu au kuchoka basi hio ni ishara nyingine ya kwamba ngozi yako inahitaji maji, Ukosefu wa maji mwilini huathiri uwezo wa ngozi yako kufanya kazi muhimu kama cell turn over, Bila unyevu wa kutosha, ngozi haitoi safu yake ya nje mara kwa mara lakini hii husababisha dead cells kujilimbikiza katika ngozi yako. Hii husababisha kuziba kwa pores na ngozi kuonekana dhaifu,

  • Mikunjo Ya Uzee

Ngozi iliyokosa maji huwa na mtindo wa kuzeeka mapema, angalia kwenye ngozi iliyozunguka macho yako, kama una mikunjo ambayo inaonekana inawezekana ni kutokana na ngozi kukosa maji. Usi-mistake mikunjo ya ku-smile na mikunjo ambayo ipo tu muda wote.

Unaweza kujua ngozi yako haina maji kwa kujifinya mashavu, kama itatokea fine lines basi moja kwa moja ngozi yako inaupungufu wa maji.

Ufanyenini Hili Kuondokana Na Tatizo Hili?

Hydrate

Kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kufanya baada ya ngozi yako kukosa maji ni kuongeza maji, unatakiwa kutumia bidhaa zenye unyevu ndani yake.

Epuka Utumiaji Wa Vilevi Na Kahawa

Hapa sio kwamba usinywe au uache kabisa bali ni kupunguza utumiaji wake, kunywa vikombe viwili vya kahawa au glass moja ya pombe kwa siku ni sawa lakini kutumia vitu hivi mara nyingi kupita kiasi ni mbaya kwa afya ya ngozi yako

Oga / Osha Uso Kwa Kutumia Maji Ya Uvuguvugu

Haya ni maji sahihi kuoshea uso wako, yanaondoa uchafu vyema lakini pia yanasaidia kuhifadhi mafuta yako ya asili ya ngozi

Maji Yapi Yanafaa Kuoshea Uso Wako?

Related posts