Tunapo sema kuwekeza katika nywele bora hapa hatumaanishi Natural Hair au Relaxed hair, hapa tunamaanisha weaving na wig’s. Wengi tunapenda kuwa na weaving na wig’s kiukweli ni life saver hasa kwa sisi ambao tuna nywele zinachokua muda kukua au hata pale unapo hitaji kutoka na nywele hazipo sawa.
Wengi tunapoteza hela kununua weaving au wig’s nyingi mara kwa mara kunatufanya tuwe tunabadilisha mionekano lakini tunakuwa tunatumia hela nyingi katika sekta hii bila sababu, utaisukia au kuivaa mara mbili mara tatu halafu haina kazi tena.
Tujifunze kwa Jacqueline Mengi kama ni mfuatiliaji wa huyu dada utajua ana weaving zake 4 tu ambazo zina quality nzuri na anauwezo wa kuzibadilisha vile anavyo penda yeye. Inawezekana utasema lakini hizi nywele ni ghali sana, well kilicho ghali ni wewe kuendelea kununua nywele za bei rahisi zisizo na ubora ni bora uwe na weaving moja ambayo ina quality nzuri unaweza kubadilisha rangi, kubadilisha style na kadhalika kuliko kila siku kununua nywele za styles na rangi tofauti.
Wakati wa kununua angalia vitu hivi muhimu kujua nywele ina quality nzuri au lah?
Angalia aina ya nywele
- Kuna aina nyingi za nywele na kuna kampuni nyingi na mbalimbali ambazo zinatengeneza nywele hizi, kutokana na demand yake kubwa sasa wengi wana jaribu kutengeneza hata zile ambazo hazina quality nzuri zionekane zina quality soma na jua vizuri ni aina ipi ya nywele una nunua kuna brazilian hair, human hair, virgin hair,indian hair, peruvian hair etc. unacho takiwa kujua ni nywele gani hasa unanunua.
Angalia ubora wa lace
- Hizi nywele huwa na lace chini, kama umesha angalia watu wengi wanao sukia nywele zisizo bora lace yao hu-shout sana au zinakuwa bonded ndivyo sivyo tofauti na quality hair lace yao inakua haionekani unless uangalie kwa makini sana na ukiisukia haileti picha mbaya.
Zinashikana?
- Ni vyema ukaenda dukani kukagua nywele yako, fanya kama unaichana kwa vidole kama vidole vinakwama jua hio sio quality hair lakini kama vinaingia na kupitiliza mpaka chini that a quality hair & your good to buy it.
Note: Another Tip is to get yourself a good hair stylist hata kama nywele itakua quality kiasi gani kama hair stylist wako ni mbaya obviously ata haribu nywele yako, wanaweza kuwa expensive lakini we always choose quality over quantity.
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you will find 54465 more Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/jacqueline-mengi-ni-mfano-mzuri-wa-kwanini-uwekeze-katika-nywele-bora/ […]