SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

JALI NGOZI YAKO KWA KUFANYA HAYA
Skin Care

JALI NGOZI YAKO KWA KUFANYA HAYA 

Wengi hudhani kujali ngozi ni kupaka mafuta au kutumia ma chemical lakini kumbe kuna vitu vichache ambavyo tuna visahau kufanya na ni muhimu sana, vitu hivyo ni kama;

BADILISHA FORONYA ZA MITO.

stack of pillows1

 

Tunapo lalia foronya kuna bacteria wengi ambao tunawaacha hivyo hata kama ukiwa una paka mafuta mazuri kiasi gani unapo rudi kulala kwenye ile foronya lazima ngozi itaharibiwa tena na wale bacteria, badilisha foronya za mito mara mbili kwa wiki.

OSHA MAKE UP ZAKO MARA MOJA KWA WIKI.

IMG_7601(1)

Kama ilivyo kwa mito basi pia ni hivyo hivyo katika make up brushes jaribu kuzifanyia usafi mara moja katika kila wiki na utaona matokeo mazuri katika ngozi yako.

OSHA USO WAKO KABLA YA KULALA.

enhanced-16444-1447180075-5

Hakikisha unaosha uso wako kwa maji masafi na sabuni kila siku kabla ya kwenda kulala, hii husaidia kuacha ngozi yako safi, kuondoa bacteria wa siku nzima na kufungua matundu yaliyo jaa vumbi au mafuta ya mwilini.

KUNYWA MAJI MENGI.

studiodiy-water

Maji ni huduma kubwa sana kwa afya sio ya mwili tu bali ya ngozi pia, jaribu kubeba chupa ya maji na unywe mara kwa mara utaona matokeo ya jinsi ambavyo ngozi yako itakavyo nawili.

EPUKA KUTUMIA MAFUTA YENYE CHEMICAL NYINGI.

theeverygirl_hairmask4

Kuna chemicals/kemikali ambazo zinaharibu ngozi, jaribu kutumia vitu vya asili kama mayai, asali au hata limao pia husaidia.

ACHA KUTUMBUA VIPELE.

spot treatment

Acha kutumbua vipele, kutumbua vipele unaweza kusababisha vidonda au madoa usoni jaribu kupaka dawa sehemu yenye kipele kuna njia nyingi kama dawa ya mswaki au hata limao inaweza kukausha kipele bila kuaharibu ngozi.

 

Related posts

Leave a Reply