SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Korean Skincare Zinaweza Kusababisha Uharibifu Wa Ngozi (Breakout)
Urembo

Je Korean Skincare Zinaweza Kusababisha Uharibifu Wa Ngozi (Breakout) 

Kwasasa skincare products ambazo zinasifika kwa uwezo wake wa kufanya ngozi kuwa nzuri na kuondoa breakout ni vipodozi vya kikorea, ambavyo inasemekana vipodozi hivi hutengenezwa asilimia kubwa na vitu vya asili na vitu ambavyo havina madhara lakini pia vinasifika kwa kuleta unywevu katika ngozi.

Japo vipodozi hivi ni vizuri na Dunia inavisifia haimaanishi basi haviwezi kukusababishia madhara katika ngozi inawezekana vikaleta madhara kama vipodozi vingine mfano:

  • Korean Skincare ni tofauti kidogo wana routine mpaka ya vipodozi 10, kama ngozi yako haijazoea na kama umenunua tu bila mpangilio na kujua kipodozi gani ninaendana na kipodozi gani basi unaweza kupata madhara.
  • Pia kuna active ingredients katika vipodozi vyao, kama uso wako haujazoea ingredients hizi pia inawezekana kupata madhara.
  • Endapo utanunua kipodozi bila kujua kama kinaendana na ngozi yako au lah, sababu tu ni Korean product haimaanishi inafaa kwa kila aina ya ngozi japo vingi vinaandikwa hivyo lakini ni vyema kujua aina ya ngozi yako na kipodozi kipi kinakufaa.
  • Kama unafikiria  kufuata utaratibu wa utunzaji wa ngozi wa Kikorea, ni muhimu kufanya utafiti wako na kupata bidhaa zinazofaa kwa aina ya ngozi yako. Anza na kiasi kidogo cha bidhaa na ongeza kadri ngozi inavyozizoea.
  • Japo vipodozi hivi vinasifika lakini tukumbuke pia swala la ngozi linatokana na unachokula pia, tunapoona wa Korea wana ngozi nzuri pia wanakula vyakula vizuri na hii inaonekana hata kwenye life span yao ni ndefu kuliko sisi, kama unatumia kipodozi cha kikorea na una kula vyakula visivyo sahihi basi pia unaweza usione matokeo mazuri.

Tuambie je ulishawahi kutumia vipodozi hivi na matokeo yake yalikuwaje?

Related posts