SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Nahitaji Kutumia Towel / Taulo Tofauti Mwilini Na Usoni?
Skin Care

Je Nahitaji Kutumia Towel / Taulo Tofauti Mwilini Na Usoni? 

Tunatumia muda mwingi katika kuhakikisha ngozi zetu zinakuwa nzuri, unakuwa na skin care routine, unaosha uso wako vyema lakini bado utakuta matokeo hayawi vile ambavyo unategemea kumbe kuna baadhi ya vitu vidogo vidogo ambavyo vinasababisha hili kimoja wapo ikiwa ni Taulo, Khanga, Kitenge au kitu chochote ambacho unatumia kufutia mwili wako pamoja na uso wako.

  • Swali Je naweza kutumia taulo moja usoni na mwilini?

Jibu ni HAPANA ni vyema kuwa na mataulo tofauti ya kujifutia usoni na mwilini. kama ambavyo tunajua taulo linapita sehemu nyingi kujifutia ikiwepo miguuni na sehemu nyeti kuna bacteria ambao unaweza kuwatoa sehemu moja na kupeleka nyingine ikaleta madhara.

  • Je Ni Kwa Kipindi Gani Nahitajika Kusafisha Taulo / Kitambaa Cha Kufutia Uso?

Unatakiwa kukisafisha kitambaa hiki mara kwa mara unapokitumia, au kutumia kipya mara baada ya kutumia kwa muda fulani eg siku mbili. Lakini hakikisha pia taulo, khanga, kitenge chako kinakauka kabla ya kukitumia tena na hii sio tu kwa kitambaa cha usoni bali hata mwilini.

  • Je Ni Kitambaa Cha Aina Gani Kinafaa Kutumia Kama Face Towel?

Kitambaa chochote ambacho ni laini, kitambaa kigumu kinaweza kusababisha michubuko, kupata wekundu katika ngozi na madhara mengine hakikisha kitambaa unachotumia ni soft na hakitaleta madhara yoyote katika ngozi yako.

MUHIMU: kama unaona kufua au kubadilisha kitambaa chako cha usoni mara kwa mara ni shida kwako basi acha uso wako ukauke kwa hewa huitaji kitaulo kukausha, hii tu sio inasaidia kuepusha usumbufu wa kufua na kubadilisha kitambaa lakini pia hufanya ngozi yako kuwa hydrated kwa sababu ngozi inanyonya maji.

Related posts