SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Ni Kweli Mtu Mweusi Haitaji Sunscreen?
Urembo

Je Ni Kweli Mtu Mweusi Haitaji Sunscreen? 

Hili ni swali ambalo wengi wetu tunajiuliza je ukiwa mweusi unahitaji suncreen? ambapo wengi wetu tunaamini kwamba kipodozi hiki ni kwa ajili ya wale wenye ngozi nyeupe tu kana kwamba sisi hatajua kilitupiga hakuna kinachobadilika.

Leo tunakupa jibu la swali hili,

Si kweli kwamba mtu mweusi haitaji kupaka sunscreen,Kila mtu anahitaji kulinda ngozi yake kutokana na mionzi ya jua, na wakati melanini ya asili hutoa ulinzi wa jua, haitoshi.

Mionzi ya UVA na UVB kutoka katika jua inawajibika kwa kufanya ngozi izeeke pamoja na kukupa sunburns, lakini pia kuna cancer ya ngozi pamoja na skin hyperpigmentation ambazo vyote hutokana na mionzi ya jua.

Matumizi ya sunscree ni muhimu kwa ngozi za aina zote iwe nyeupe, nyeusi au maji ya kunde, inasaidia kuweka kizuizi kati ya jua na ngozi yako na kukuepusha na maradhi na uharibifu wa ngozi.

Related posts