SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Ni Sawa Kuvaa Kikuku Ofisini?
Urembo

Je Ni Sawa Kuvaa Kikuku Ofisini? 

Ikiwa accessories ni moja ya namna ya kunyanyua muonekano wako hasa kwa mavazi ya ofisini ambayo kuna muda yanaweza kuonekana too boring, lakini huwezi kuvaa tu accessory yoyote kazini kuna ambazo zinafaa na ambazo hazifai.

Week iliyopita tulitoa tips kadhaa kuhusu accessories za kuvaa kazini, week hii tunataka kujibu hili swali na kwasababu tumeona baadhi ya watu wakivaa vikuku (anklet) ofisini.

KIkuku hakifai kuvaa kazini, yes kiwe gold, silver, cha shanga chochote haifai kuvaa kazini, kutokana na kwamba kikuku vina draw attention kwenye miguu, utafanya wengine washindwe ku-concetrate na kuwa wanakuangalia miguuni.

Tayari kikuku kinasifa mbaya hasa kwetu Africa (japo si kweli) lakini huitaji kuwa topic huko makazini na kama boss wako ni old fashioned unaweza kusababisha uonekane mtu asiejielewa wakati hilii si lengo lako.

Kikuku kinaweza kushusha vazi, ndio maana unaweza kuona hata mavazi ya harusini au kwenye mitoko kama red carpet watu hawavai vikuku, hata kama ni cha thamani hakifai kuvaliwa kwenye mavazi ambayo ni official na ya mitoko.

Lakini unaweza kuvaa endapo tu kama kazi yako ina ruhusu hasa wale ambao wanafanya casual work.

Tupe maoni yako kuhusu hili.

Related posts