SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Cream Mask Inavyoweza Kukuokoa Na Uzee Wewe mwenye miaka 45+
Skin Care

Jinsi Cream Mask Inavyoweza Kukuokoa Na Uzee Wewe mwenye miaka 45+ 

Je umefatilia sehemu ya kwanza ya kufahamu kuhusu mask. Kama bado pitia uone jinsi peel off mask inavyoweza kuondoa blackheads “vichwa vyeusi”, na whiteheads “vichwa vyeupe”.

  • Leo tunaendelea na Sheet mask

Sheet mask ndio mask pekee inayoweza kutumiwa na karibu kila mtu na kizuri zaidi mask hii zipo za sehemu tofauti tofauti maalum kwa ajili yako. Zipo kwa ajili ya Macho, pua, midomo na miguu pamoja na nywele na pia na uso wote. Hii inaongeza unyevu nyevu kwenye ngozi yako.
Sheet mask zinapatikana katika maduka ya urembo na vipodozi. Original yake ikiwa ni korea kusini. Kwenye swala la gharama mask hii inaanzia $1 hadi $20 kutegemeana na malighafi iliyotumika kutengeza mask hiyo.


Cream mask Kama una ngozi kavu na unahitaji unyevunyevu katika ngozi yako na kuondoa ukavu mask hii ni kwa ajili yako. Cream mask inawafaa wazee wale umri ambao umeenda kidogo.  Pia ni tiba nzuri kwa wenye ngozi mchanganyiko na yenye madoa.

  • Gel Mask 

Inakufaa hasa kama una ngozi kavu na iliyokauka inaongeza unyevu nyevu ambao utaondoa ukavu wote.
Sleep MaskHii ni kwa ajili yako wewe unaetaka kuongeza unyevunyevu kwenye uso wako na kuondoa ukavu. Hutumika zaidi muda mchache kabla ya kulala na unalala nayo.

  • Clay (Mud)

Mask Hii ni mask ya udongo imekuwepo katika sekta ya urembo kwa muda mrefu kuna aina chache za clay mask ikiwa bentonite na kaolin clay ndio zinazojulikana zaidi aina zote za clay ni nzuri zinaondoa sumu kwa kuinyonya yote nje ni nzuri zaidi kwa wewe ulie na ngozi yenye chunusi sugu. L’oreal paris inatwaja kuwa ni brand maarufu zaidi wenye clay mask nzuri kwa matumizi ya ngozi.

  • Cream Mask

Kama una ngozi kavu na unahitaji kuongeza unyevunyevu mask hii ni kwa ajili yako. Cream mask pia inawafaa zaidi wale umri ulioenda zaidi “45+”. Hii pia inakufaa kama una ngozi mchanganyiko na una madoa mengi usoni.

  • Charcoal Mask

Hapa kuna utofauti kidogo, unaweza kukutana na Peel off mask, sheet mask, cream mask, na mud mask zote ikiwa na active ingredient ya Charcoal hii ni kwa ajili ya wewe mwenye ngozi ya mafuta kwa ajili ya kusafisha ngozi na chunusi sugu.


Unapojaribu Mask kwa Mara ya Kwanza: Fanya majaribio chini ya sikio lako hutapenda kuona unapata reaction baada tu ya kupaka uso mzima kwa mara ya kwanza. Majaribio hayo yatakusaidia kuona kama hiyo mask inafaa kwa ngozi yako au haifai. Na Tumia kama maelekezo yanavyosema kutoka kwa mtengenezaji.
Jee wewe unapenda kutumia mask ya aina gani zaidi?
©️binturembo

Related posts

1 Comment

  1. Buy DMT Vape pen for Sale Australia

    … [Trackback]

    […] There you will find 13234 more Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-cream-mask-inavyoweza-kukuokoa-na-uzee-wewe-mwenye-miaka-45/ […]

Comments are closed.