SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Peel Off Mask Inavyoweza Kuondoa Blackheads
Skin Care

Jinsi Peel Off Mask Inavyoweza Kuondoa Blackheads 

Mask ni hatua ya kutunza ngozi yako ambayo Unaifanya kwa wiki Mara moja. Na unafanya baada ya kufanya scrub/ exfoliation. 
Unapochagua mask unatakiwa kuzingatia Aina yako ya ngozi, umri wako na mahitaji yako.


Kuna Aina Saba za mask na kila mask ina kazi yake na ni maalum kwa wenye ngozi Aina yake na mahitaji pia.


1. Peel off mask 

2. Sheet mask 

3. Hydrating mask

 4. Cream Mask 

5. Clay (mud)  mask

 6. Gel Mask 

7. Sleep Mask


Kazi ya Mask kwenye ngozi ni Kama ifuatavyo:
1. Inanyonya mafuta yaliyozidi usoni 

2. Inaondoa uchafu wa ndani zaidi na ngozi iloyokufa 

3. Inaongeza unyevunyevu kwenye ngozi 

4. Inaondoa vichwa vyeusi “blackheads” na vichwa vyeupe “Whiteheads”5. Inaondoa mistari ya uzee Pamoja na makunyazi.


Kumbuka mask ni hatua kwenye utaratibu wa kutunza ngozi hivyo inaenda kufanya kazi yake kama tu upo kwenye routine na unaendelea Nayo vizuri. 

  • Peel off mask. 

Kwa Leo tuanze kujifunza Kuhusu peel off mask. Hii ni mask ya kumenya.
Inawafaa wenye ngozi ya mafuta, na ni kwa ajili ya kutoa uchafu kwenye ngozi Pamoja na ngozi iloyokufa. Mask hii inawafaa wenye chunusi zisizoisha, wenye vichwa vyeusi na vichwa vyeupe. Na wenye madoa usoni.
Peel off mask ambazo zitasaidia kukisafisha uso kutoa blackheads usoni ,na mafuta mafuta na uchafu wote,na kukuacha na ngozi safi kabisa.
Peel off mask Zipo zinauzwa madukani ready made pia Zipo DIY Unaweza kufanya nyumbani kama zifuatazo 


1. Asali na Maziwa mabichi.

Changanya Maziwa mabichi kiasi na asali kwa kiwango kinachofanana.Paka usoni baada ya muda . Utamenya kuanzia kidevuni kuja juu. 


2. Ute wa yai na limau. 

Chukua Ute wa yai moja na limau kipande. Changanya na weka usoni. Baada ya dakika 5 Utamenya na utaosha uso wako.

 
3. Gelatine ,Unga wa Mkaa Na Maziwa ya Moto.

Gelatine vijiko viwili,unga wa mkaa vijiko viwili na maziwa ya moto Changanya Upate mchanganyiko vizuri. Gelatine Ndio inaleta sifa ya mask kuwa peel off.  
Changanya Upate mchanganyiko, Kisha paka usoni baada ya muda menya kuanzia kidevuni kuja juu. Usishushe chini, unashusha ngozi. 
Gelatin Inapatikana madukani.
Tahadhari : Tumia mask kulingana na mahitaji yako kwa matokeo bora. 

©binturembo

Related posts

3 Comments

  1. mushroom candies

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-peel-off-mask-inavyoweza-kuondoa-blackheads/ […]

  2. Where to Buy Changa DMT online Brisbane

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-peel-off-mask-inavyoweza-kuondoa-blackheads/ […]

  3. top article

    … [Trackback]

    […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-peel-off-mask-inavyoweza-kuondoa-blackheads/ […]

Comments are closed.