SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

JINSI YA KUFANYA CONTOURING WAKATI WA KUFANYA MAKE UP
Make Up

JINSI YA KUFANYA CONTOURING WAKATI WA KUFANYA MAKE UP 

Kupaka makeup kumekua ni kitu cha kawaida na kinachopendelewa na watu wa rika tofauti. Kuna mbinu mbalimbali za kufanya makeup na moja wapo ni Contouring na leo make up artist @flawlessfacesbysoso anakuletea mbinu hizo za kupaka contour


Contouring ni moja ya mbinu ya kufanya make up ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuchonga baadhi ya sehemu ya uso na kuifanya sura kuwa defined zaidi na pia kubadili muonekano wa viungo kwa usoni kutegemea na jinsi mtu anavyopenda. Mfano kuchonga pua ionekane nyembamba zaidi ya ilivyo, lips zionekane kubwa zaidi au hata sura ionekane nyembamba au nene kuliko kawaida. Hii inategemea na mapenzi ya mtu na jinsi gani anataka aonekane.

 

Kama inavyojulikana, kila mtu ana rangi yake ya mwili. Mbinu hii ya contouring inabidi kutumia foundation ama concealer ambayo ni ya giza zaidi kuliko rangi ya mwili wako ama ile ambayo inafanana na foundation uliyopaka mwanzoni (foundation inatakiwa ifanane na rangi ya ngozi).
Countouring inaenda sambamba na highlighting, ambapo kwenye highlighting inatumika concealer ambayo ina nuru (light) mara moja au mbili zaidi ya rangi ya ngozi yako. Hii yote hi kuweka mwanga baadhi ya sehemu ya uso.

Hizi ni sehemu contour inapofanyika na jinsi inayoweza kubadili sura:

Pua: Inafanya pua ionekane ndefu zaidi. HaipendezI kuzidisha sana contour kwenye pua maana itapoteza uhalisia.
Kwenye mashavu/Cheekbones: inafanya sura ionekane nyembamba zaidi.
Taya (Jaw): uki Contour taya inashape sura na kufanya mtu alieongezea unene wa sura kuonekana nyembamba na kuchonga zaidi.
Sehemu nyingine ni kama zinavyoonekana kwenye picha, wapi pa ku highlight na wapi pa kucontour

 

Ni muhimu pia kujua muundo wa uso wako kwa kabla haujafanya Countoring na Highlighting. Hii ni  kwasababu sura zinatofautiana muundo.

Jinsi Ya ku-Contour kulingana na muundo wa sura yako

Cha muhimu pia wakati wa contouring na highlighting ni ku blend (kuchanganya) vizuri concealer uliotumia pale unapoipaka usoni kwa kutumia beauty blender au brush, ili kuzuia sura isionekane kama ina matope na kuleta uhalisia wa sura yako.

 

Related posts