Kuna vitu vinaweza kukufanya usiwe comfortable kuvaa mavazi ya aina fulani kutokana tu na kuwa na kasoro au kitu kidogo sehemu hio na labda una shindwa kuomba ushauri ufanye nini kutokana na sehemu hio kuwa ya siri kidogo. Mfano mzuri ni wengi kuogopa kuvaa body suits au bikini beach kwa sababu ya rangi ya makalio yao kutokuwa sawa na rangi ya mwili, yaani makalio mara nyingi huwa meusi kuliko mwili hii inaitwa sugu za makalio hutokana na kukaa sana lakini pia huwa hatutilii maanani kusafisha ngozi ya eneo hili kama ambavyo tunasafisha sehemu nyingine.
Je inawezekana kutakatisha kalio na kurudi katika rangi ya kawaida? ndio na hivi ndivyo utahitajika kufanya
- Unga wa mchele – unga wa mchele unasifika kwa uwezo wa kuondoa dead skin layers na kuleta ngozi mpya inayo vutia, pia husifika katika kung’aza ngozi
- Asali – husifika sana katika urembo hasa katika kung’arisha na kufanya ngozi iwe nyororo lakini pia husifika katika kuondoa chunusi.
- Limao – ni kama asali, huondoa chunusi, kung’aza ngozi.
- mafuta ya nazi – kuifanya ngozi kuwa soft & smooth.
Mahitaji
- unga wa mchele – vijiko vitatu
- asali – kijiko kimoja
- limao – juice ya limao kijiko kimoja
- mafuta ya nazi – kijiko kimoja
Namna ya kuandaa na kufanya
- changanya mahitaji yako kwa pamoja katika bakuli/chomcbo chochote utakacho weza kuchanganya mchanganyiko wako
- changanya vizuri vichanganyike kwa pamoja na upate uji wa mahitaji yako
- paka kwenye makalio na uache ikae kwa dakika 5
- massage na futa / osha makalio yako
- fanya hivi kila siku kabla ya kwenda kuoga
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuonda-sugu-za-makalio/ […]
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuonda-sugu-za-makalio/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuonda-sugu-za-makalio/ […]