Jinsi ya kuondoa nywele za usoni au ndevu kwa wanawake.
Leo kwenye urembo tutaongelea jinsi ya kuondoa nywele za usoni pamoja na ndevu ambazo siku hizi wanawake wengi wamejikuta wana nywele  ambazo zinawakera.


Kwa kutumia kiwembe inaweza kuwa ni rahisi sana kwani ni kitu cha dakika lakini ujue nywele hizo zitarudi haraka sana.
Hapa nimekuletea vitu asilia ambavyo vinaweza kukuondolea nywele hizo na ukakaa kwa muda mrefu bila kuziona na usipate madhara ya mapele kama ambavyo ungenyoa na kiwembe.

Mahitaji:

  • Vijiko viwili vya asali.Kijiko kimoja cha ngano.Vijiko viwili vya juisi ya limao.
  • Chukua ngano isage mpaka upate unga wake. Changanya na asali pamoja na limao baada ya hapo paka kwenye eneo lenye nywele ukimaliza acha kwa muda wa dakika 15 kisha osha na maji ya vuguvugu.
  • Baada ya hapo paka kipako chako rudia kupaka mchanganyiko huu mara mbili mpaka tatu kwa wiki ndani ya mwezi mmoja utaona nywele hizo zimepotea kabisa.

Kama una ngozi laini isiyotaka mikikimiki jaribu kidogo ili isije kukuletea matatizo.

©binturembo