SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kuondokana Na Vipele Baada Ya Kunyoa Sehemu Za Siri
Skin Care

Jinsi Ya Kuondokana Na Vipele Baada Ya Kunyoa Sehemu Za Siri 

Nini Umuhimu wa hizo nywele sehemu za Siri ?


Nywele za uke na uume huzuia maambukizi ya bakteria ambao huweza kupenya kwenye vitundu vidogo vya sehemu hizo,vilevile huzuia mchubuko wa ngozi katika sehemu hizo.
Sababu hii haimaanishi usinyoe sehemu za Siri. Sehem hizi zikizidi nywele hutoa harufu mbaya. Hivyo zingatia husafi na unadhifu pia.

SABABU ZA KUTOKEA VIPELE HIVYO. 
Sababu zipo nyingi. Baadhi ambazo ni sababu kwa wengi ni kama:

 • Urudiaji wa kiwembe ulichokwisha kukitumia uliponyoa kabla ya siku hiyo au kutumia kiwembe butu kama njia ya kunyolea.
 • Kunyoa uelekeo tofauti na nywele zako zinavyoota.

Nini nifanye baada ya kupata vipele?

Mara nyingi vipele hivi hupotea vyenyewe baada ya muda, Ila kuna vingine huwepo kwa muda mrefu na hata kuanza kuuma na kutengeneza usaha. Baadhi ya njia husaidia ni kama:

 • Kutumia kitambaa safi na maji ya vuguvugu kukanda sehemu iliyo na tatizo hilo.
 • Matumizi ya asali na maji ya vuguvugu pia husaidia kupunguza vimelea vya bakteria wowote katika eneo hilo na hupunguza vipele hivyo
 • Matumizi ya yai. Yai linaprotini ziitwazo albumin ambazo husaidia sana ngozi.kwahyo husaidia kuponesha ngozi yenye vidonda au vipele kwa haraka.unatumia sehemu ya nje (nyeupe) ya yai kupaka sehemu husika unaacha inakaukia hapo halafu unabandua,inatoka pamoja na kipele hasa kilichoanza kutunga usaha.
 • Matumizi ya sukari kama scrub. Sukari ina glycolic acid ambayo hupenya kwenye ngozi na kusaidia kuua seli zilizokufa na kuponya ngozi iliyoharibika eneo hilo haraka. Jinsi ya kutumia?Changanya sukari na mafuta ya olive kama unayo, kama huna tumia ata ya nazi kisha paka sehemu husika na sugua taratibu kwa kuzungusha taratibu kuelekea juu kisha acha kwa muda. Alafu toa kwa maji ya vuguvugu. Rudia hivi hadi vitakavyokwisha.

Endapo njia hizi hazikusaidii, muone daktari wa ngozi kwa matibabu sahihi zaidi.

Nini nifanye kuzuia vipele hivi?

 •  Kwanza tumia maji ya vuguvugu ulowanishe sehemu hiyo unayonyoa, kisha tumia sabuni/shaver cream kuweka povu la kutosha ili unyoe kirahisi zaidi kwa maana nywele zinaasili ya kuota kwa kujifungafunga na ni ngumu pia, hivyo kwa kulainisha hupunguza uwezekano wa kupata vipele.
 • Baada ya kulainisha nyoa kwa kutumia kiwembe/mashine ya kunyolea mpya kwa uwelekeo ambao nywele zako huota.
 • Baada ya kunyoa ni vyema kutumia aftershave ambayo husaidia kuzuia bakteria ambao wanaweza kupenya kwenye vitundu vidogo baada ya kunyoa.

Vilevile imeelezwa kuwa hupaswi kunyoa nywele zote za uke au uume na kuacha kipara, kwasababu huongeza hatari za magonjwa ya ngono wakati wa tendo la ndoa majimaji na bakteria huweza kupenya kutokana na vitundu vidogo vinavyokuwepo baada kunyoa nywele zote.

Muone daktari endapo hali hii haiishi na haswa vipele vikiendelea kutokea, vinatoa usaha, vinauma sana na vinakuwa vyekundu

By @binturembo

Related posts

1 Comment

 1. สล็อตเว็บตรง แตกง่าย

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuondokana-na-vipele-baada-ya-kunyoa-sehemu-za-siri/ […]

Comments are closed.