SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kuondokana Na Whiteheads ” Vipele Vyeupe Puani “
Skin Care

Jinsi Ya Kuondokana Na Whiteheads ” Vipele Vyeupe Puani “ 

ivo vitu vyeupe ni Ngozi iloyokufa “Dead  skins” ambazo zikikutana na hewa sinafanya kama upele fulani hivi au tunaita whiteheads.
Whiteheads ” vichwa vyeupe” ni aina ya chunusi na huwatokea zaidi wenye ngozi ya mafuta, wanawake na wanaume,  wazee kwa vijana. 


Unaweza kuviondoa kwa kutumia facial cleansers na oil free moisturizer(cream). Osha uso mara mbili kwa siku na maji ya vuguvugu.
Baada ya kuosha fanya kama unapigapiga taulo usoni “pat dry” usisugue. Hii ni njia inayopunguza uchafu na mafuta kujijenga kwenye skin pores.
Tumia Face cleanser ambayo itaondoa uchafu na dead skin Zote kwenye ngozi.
Bidhaa za vipodozi vyenye viambata kama alpha-hydorxyl acid,salicylic acid au benzoyl-peroxide ni nzuri kwa kuondoa hivo vitu. Ulizia Maduka ya vipodozi vyenye kuaminika utavipata.


Steaming ni njia nzuri ya kuondoa white heads.Chemsha maji moto weka kwenye bakuli,acha ule mvuke ukupige usoni kwa dakika 15.
Steaming ni njia nzuri ya kufungua tundu za kwenye ngozi,ambapo inakuwa kwa urahisi kuondoa uchafu kwenye ngozi.


Tumia scurbs kulingana na ngozi yako hii Inaondoa ngozi iloyokufa na kusafisha ngozi.
Ukitoka kuoga tumia vidole vyako viwili kusugua taratibu eneo la pua ,itaondoa ngozi zote zilizokauka.


Epuka kujishika eneo hilo wakati wote,kwasababu vijidudu vilivyopo kwenye mikono vinasababisha muongezeko wa hali hio.


Kuna njia mbadala pia ambazo zinaweza kutumia nyumbani kuondoa hizo whiteheads.

 • Aloevera

Ni anti-septic(inaua vijidudu) in nature na ina anti-oxidants. Changanya drop 3 za juisi ya limau na aloevera gel. Weka kwenye uso,kisha sugua taratibu kwa dakika 15,suuza uso na maji moto.

 • Nyanya

Nyanya inasemekana kuwa leukopene ambayo ina uchachu unaosaidia kuondoa whiteheads. Tengeneza juisi ya nyanya,chukua hii juisi na uweke usoni mpaka ikauke. Suuza uso kwa maji ya vuguvugu.

 • Asali

Pasha moto asali yaani kwenye waterbath, ikiwa na joto la kiasi sio la kuunguza,weka usoni na usugue taratibu kwenye eneo la pua kwa dakika 10,kisha acha ikauke. Suuza inapokauka.

 • Sugar Scrub

Saga sukari iwe powder. Changanya na juisi ya limau, weka kwenye eneo la pua na scrub Kisha sugua taratibu. Baada ya dakika 20 osha. 

 • Mayai

Mayai yana omega-3 fatacids nyingi, vitamins na minerals ambazo zinamea ngozi. Chukua ule weupe  wa yai weka kwenye uso,ukishakauka suuza na maji ya vuguvugu.

by @binturembo

Related posts

1 Comment

 1. Iowa Hawkeyes Shop

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuondokana-na-whiteheads-vipele-vyeupe-puani/ […]

Comments are closed.