SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi ya kupata (Ngozi mtelezo) Flawless Skin
Skin Care

Jinsi ya kupata (Ngozi mtelezo) Flawless Skin 

Kuna watu ni wazuri jamani ila uzuri wao hauonekani sababu ngozi zao zipo rough sana, ubora  wa ngozi ni matokeo ya mambo mengi sana ,najua kufanya yote kwa sisi tulio busy ni ngumu kidogo , ila ukifanya japo mawili matatu utanawirika tu.

Nakukumbusha mambo hayo ya msingi ni  kula vizuri mbogamboga na matunda, kunywa maji mengi na kusafisha uso kwa vitu asilia angalau mara moja kwa wiki. Zipo njia nyingi sana za kusafisha ngozi kiasili. Leo nitakupa moja na ukiifanya ipasavyo haitokuangusha.

Nitatenganisha jinsi ya kusafisha ngozi ya mafuta na zile ngozi za kawaida na kavu. Kama huijui aina ya ngozi yako , Soma andiko hapo chini litakusaidia


KWA NGOZI YA MAFUTA


Mahitaji

 • Ute wa yai
 • kipande cha  limao
 • manjano kijiko kimoja 


Jinsi ya kufanya

 • Changanya vitu vyote katika chombo kimoja
 • kisha osha uso na sabuni isiyo na kemikali
 • jikaushe kisha paka mchanganyiko wako usoni kaa nao kwa dakika 20 hadi 30 kisha osha
 • Ili kuzuia ngozi isiwe kavu Sana ,paka moisturizer unayotumia.


KWA NGOZI KAVU NA YA KAWAIDA


Mahitaji

 • Kiini cha yai
 • maziwa fresh
 • Manjano kijiko kimoja


Jinsi ya kufanya 

 • Changanya vitu vyote katika chombo kimoja
 • kisha osha uso na sabuni isiyo na kemikali
 • jikaushe kisha paka mchanganyiko wako usoni.kaa nao kwa dakika 20 hadi 30 kisha osha.


Ili kuzuia ngozi isiwe kavu Sana ,paka moisturizer unayotumia.


©binturembo

Related posts

1 Comment

 1. pg slot

  … [Trackback]

  […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kupata-ngozi-mtelezo-flawless-skin/ […]

Comments are closed.