SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kutumia Tango Kuilainisha  Ngozi
Skin Care

Jinsi Ya Kutumia Tango Kuilainisha Ngozi 

Tango ni tunda muhimu sana katika kusaidia afya na uzuri wa ngozi. Unaweza kula tunda lenyewe, kupaka juisi yake, kugandika vipande vyake vidogo vidogo au kunywa juisi yake. Njia zote hizo zinakusaidia kupata virutubisho muhimu kwa ngozi yako.

Tango husaidia sana kulainisha ngozi na kuikaza ngozi iliyonyauka na kulegea. Yaani hufanya kazi ya Skin Tonning ya asili. Pia ukiitumia kwa muda endelevu husaidia kuondoa na kuzuia chunusi kubwa kubwa (Pimples), makovu ya chunusi, makunyanzi na ukavu wa ngozi ya usoni.
Ni moja kati ya tunda muhimu sana kwa ajili ya matundo na upendezeshaji wa ngozi yako.

Jinsi Ya Kuandaa Na Kutumia Tango Vizuri

  • Andaa tango, maji, chombo cha kuwekea vipande vya tango na kifaa cha kukatia tango (Grater) lako katika vipande vidogo vidogo na laini  Osha tango lako, chombo chako na kifaa chako cha kukatia tango lako.
  • Bila kumenya, anza kulikatakata tango lako katika vipande vidogo vidogo sana na laini na kuweka kwenye chombo chako Ukimaliza kukata tango lako chukua vipande hivyo vidogo vidogo na laini kisha paka usoni, kuzunguka macho na shingoni pamoja na juisi yake 
  • Acha ikae kwa dakika 15 – 20 na kisha nawa kwa maji na uache bila kujikausha.
  • Rudia hivyo kila siku na kwa muda endelevu hadi matokeo yatakapokuwa mazuri

Faida Za Kufanya Hivi Ni

  • rahisi sana na salama
  • Ufanisi wake ni mkubwa
  • Gharama yake ni nafuu


Ushauri

  • Tumia matango mazuri na kata kata vizuri vipande vyako.
  • Hakikisha unatumia mara tu baada ya kutengeneza, usilaze wala kutumia vipande vilivyolala. Kuwa mvumilivu kidogo, utaanza kuona matokeo mazuri baada ya wiki mbili.
  • Kama unapenda vipodozi vya asili basi tango ni zuri sana kwako. Kula tango, kunywa juisi ya tango, paka vipande na juisi ya matango.

©binturembo 

Related posts

2 Comments

  1. how long does shrooms take to kick in

    … [Trackback]

    […] There you can find 67406 more Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutumia-tango-kuilainisha-ngozi/ […]

  2. pg사

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutumia-tango-kuilainisha-ngozi/ […]

Comments are closed.