Jee Wajua? Ngozi inayozunguka jicho ni laini zaidi ukilinganisha na ngozi ya uso wako wote. Najua ulikuwa hutambui kuhusu hili na Umetoka kujigusa ndani ya dakika chache. Nina uhakika umehakikisha kwa mikono yako!
Hizi hapa ni dondoo muhimu Jinsi ya kutunza Ngozi inayozunguka jicho lako.
Ngozi yako inayozunguka jicho ni sehemu muhimu sana kwani ina ulaini na inahitaji uangalifu mkubwa. Sehemu hii ya ngozi ni nyembamba mno na inaweza kupata madhara na kitu kidogo kabisa ili hali inaweza kuzeeka mapema kabisa kabla ya muda wake.
Ndio kusema lazima ufanye mambo fulani kila siku, mchana na usiku, ili kuhakikisha kwamba sehemu hii inabaki vyema kama inavyostahili.
- Swala la kwanza muhimu ni kwamba ni lazima uoshe vitu vyote ulivyotumia kuremba jicho lako kwa kutumia visafishaji ambavyo si vikali. Bidhaa nyingi zinazotengenezwa kuondoa make up katika jicho zimetengenezwa katika mazingira ya kuhakikisha kwamba ngozi inabaki hai na isiyokuwa na matatizo.
- Inatakiwa kila asubuhi unapoamka asubuhi ni vyema ukaanza na eye gel au krimu yenye unyevunyevu na unapoenda kulala wakati wa usiku. Kwa kuwa umri unavyozidi kuongezeka ngozi huacha kujirejesha inavyotakiwa na huondoa ule ulaini wake iliokuwa nao kwanza kuhakikisha kwamba eneo hilo lina unyenyevu husaidia kuweka ngozi ile katika hali bora zaidi.

- Ni vyema ukahakikisha kwamba moisturizers unayotumia ina SPF(Sun Protecting Factor) kuanzia 30 hadi 50 ili kuhakikisha kwamba ngozi inayozunguka jicho inahamiwa vyema dhidi ya mikunjo inayosababishwa na miale ya jua.
- Njia nzuri pia ya kupunguza uvimbe wa macho ni kuweka mask kuzunguka jicho.Pia unaweza kumasaji eneo hili ili kuondoa sumu ambayo imejijenga katika mfumo wa tezi. Watu wengine huhifadhi eye cream kwenye friji na kutumia kumasaji eneo hilo ili kuondoa mauamivu yanayokuwepo.
- Tatizo la mikunjo katika ngozi inaweza kudhibitiwa kwa akutumia bidhaa za urembo zenye asidi ya glycolic ambayo pia hujulikana kama alpha hydroxy acid au AHA.
- Kuna njia pia za asilia mbazo zinaweza kusaidia kuweka sawa ngozi inayozunguka jicho kama vipande vya matango.
Mahitaji
- Tango moja kubwa
- Kata tango lako kwenye vipande vidogo vya duara, weka kwenye friji vipate baridi kwa dakika 15 ( sio lazima). Kisha weka machoni.
- Fanya hivi kila siku mara moja. Ngozi ya jicho lako Itakuwa na afya na utaondoa Weusi wa jicho.
- Pia unaweza kutumia mafuta olive oil kuzunguka macho yako kila siku na utaona matokeo yake yatakavyokuwa bora. Mafuta ya Olive yatakuondolea ukavu kwenye ngozi inayozunguka jicho lako!
Shea na uwapendao!
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-inayozunguka-jicho-lako/ […]