SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kutunza Ngozi Kilasiku ( Skin Care Routine) – 2
Skin Care

Jinsi Ya Kutunza Ngozi Kilasiku ( Skin Care Routine) – 2 

Week iliyopita tulipata kujua kuhusu namna ambavyo unaweza kutunza ngozi yako, ambapo tulianza na kuongelea kuhusu cleansing, lakini kuna step tatu ambazo inabidi uzifuate katika utunzaji wa ngozi yako kila siku nayo ni Cleanser, Tonning na Moisturizing. Leo tutajua face toner ni nini na namna ambavyo unaweza kufanya face toner.

Face toner is basically an in-between skin-care step, baada ya kuosha uso wako kabla ya kupaka mafuta (moisturizer)  step inayofuata ndio huitwa facial toning, zimetengenezwa kwa ajili ya ku-re-balance skin baada ya kuosha uso wako kwa kutumia sabuni kali au cleanser, yaani hii huifanya ngozi yako irudi katika hali yake ya awali baada ya kuiosha na sabuni au cleanser zenye kemikali na kabla hujapaka mafuta.

Toners ni muhimu zaidi  kwa watu walio na ngozi ya mafuta, au watu wanaotumia vitu vya ziada kama makeup au bidhaa nyingine za ngozi kama sun screen, lakini pia zipo kwa ajili ya kila aina ya ngozi kama ngozi kavu, sensitive skin na aina nyingine za ngozi, cha muhimu ni kujua aina ya ngozi yako na kujua toner ipi inakufaa. 

Faida Nyingine za Toner Ni

  • Inarudisha usawa wa Hp katika ngozi yako

Kawaida ngozi yetu ni acidic,  pH balance katika ngozi zetu ni kati ya tano na sita (kwa kiwango cha 0 hadi 14). Lakini usawa huo unaweza kutolewa baada ya kuosha ngozi zetu kwa kutumia sabuni zenye kemikali kali, ili ngozi kurudi katika hali yake ya kawaida huchukua muda kidogo lakini kutumia toner inaweza kusaidia kurejesha usawa huu haraka.

  • Inaongeza safu ya ulinzi katika ngozi.

Toner husaidia kuziba mashimo ya chunusi au yaliyo achwa wazi baada ya kuosha uso wako, hii husaidia kupunguza kupenya kwa uchafu katika matundu hayo na kusababisha uharibufu wa ngozi kwa chunusi au magonjwa ya ngozi.

  • Husaidia kupunguza mafuta kwenye ngozi mafuta, na kuongeza unyevu kwenye ngozi kavu

kwa ngozi ya mafuta inaweza kuwa na viungo vinavyopunguza uzalishaji wa mafuta, wakati toner kwa ngozi kavu inaweza kuwa na viungo vingi vya maji na kusaidia kuongeza unyevu katika ngozi yako.

Namna Ya Kutumia Face Toner 

Kutumia face toner ni rahisi sana, unaweza kutumia pamba kwa kumiminia face toner kwenye pamba na kupaka usoni, kwenye masikio ,shingo na kifua,  au kwa kutumia viganja vyako vya mikono. unapaswa kutumia toner baada ya kuosha uso wako, na kabla ya kutumia serum au moisturizer.

Toners inaweza kutumika mara mbili kila siku baada ya kusafisha uso wako.

Related posts

1 Comment

  1. สล็อต W88

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine-2/ […]

Comments are closed.