leo tupo kwenye hatua ya mwisho ya skin care routine, ambapo tulishaangalia kuhusu cleanser, Tonning na leo tupo kwenye step ya mwisho iitwayo moisturizing ( hapa ni kuipa ngozi yako unyevu). Hii ndio step ambayo wengi wetu tunaijua na kuipenda sana, tatizo letu kubwa ni kutokujua nini tutumie kama moisturizer (mafuta ya ngozi), mara nyingi tunatumia watu kuuliza wanatumia kipodozi gani na sisi tunaenda kununua hikohiko na kukitumia bila kujali labda mwenzio ana aina tofauti ya ngozi na yako.
Jambo la kwanza unalotakiwa kujua ni aina ya ngozi yako na vipodozi gani vinakufaa, Kila aina ya ngozi inavipodozi vyake na ni tofauti na aina nyingine ya ngozi. Ukishajua aina ya ngozi uliyo nayo jaribu kuangalia ingredients na expiration date ya kipodozi hiko, usinunue tu bila kuangalia vitu hivi viwili unaweza kuwa na allergy nacho au kama ime expire unaweza kupata matatizo ya ngozi.
Kwanini upake mafuta ngozi yako?
- Mafuta husaidia kuilinda ngozi yako na mazingira
Unaweza kusangaa ngozi ilindwe na mazingira? yes unapo paka mafuta yana virutubisho vya kuzia jua hii husaidia kukuepusha na kuharibika kwa ngozi, vumbi ambazo zikiingia kwenye ngozi husababisha chunusi na husaidia kukulinda na mazingira mengine hatarishi ambayo yanaweza kuharibu ngozi yako
- Kuipa ngozi yako afya
Katika mafuta kuna virutisho mbalimbali ambavyo husaidia kujenga ngozi yako, kuipa afya, kuifanya iwe nyororo, comfortable na attractive kama wewe ni mmoja kati ya ambao unaulizwa unatumia kipodozi gani basi jua ni kwasababu ngozi yako ina afya na inavutia.
- Kuipa ngozi unyevu
Mafuta husaidia kuipa ngozi yako unyevu ambao husaidia kulisha na kuboresha ngozi yako kwa njia kadhaa kama
Kuondoa mafuta na kuifanya ngozi yako iwe nzuri kwa asili
Kufunika na kulinda fissures ndogo katika ngozi yako
Inajenga safu ya ulinzi wa kulinda ngozi kutoka mazingira yenye uharibifu
Tumemaliza kuhusu njia tatu za kutunza ngozi yako kila siku kama kuna mada ambayo ungependa iongelewe baada ya hii usisite kutuandikia hapo chini, kama ulipitwa na njia ya kwanza na ya pili tumekuwekea link hapo chini pia..
- Jinsi Ya Kutunza Ngozi Kilasiku ( Skin Care Routine)
- Jinsi Ya Kutunza Ngozi Kilasiku ( Skin Care Routine) – 2
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine-3/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine-3/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine-3/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine-3/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 93140 additional Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine-3/ […]