SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kutunza Ngozi Kilasiku ( Skin Care Routine)
Habari

Jinsi Ya Kutunza Ngozi Kilasiku ( Skin Care Routine) 

Ngozi bora na nzuri  sio tu suala la DNA bali pia ina uhusiano na tabia zako za kila siku, tabia zako , zina athari kubwa kwa kile unachokiona kwenye kioo. Kuna vipodozi aina mbalimbali na vipo vingi vya kila brand, wengi wanasema hiki ni bora au kile ni bora, haya makelele yanaweza kusababisha ukawa unatumia vipodozi vingi na baadae ukapata athari katika ngozi yako. Unachotakiwa kujua na kufuatilia ni namna ya kutunza ngozi yako kila siku, nini cha maana kuwa na nacho na kipi uachane nacho, well leo tunakuletea vitu muhimu vya kuwa navyo na kuvifanya katika your daily skin care routine 

  • Cleansing — Kuosha uso wako 
  • Toning — kusawazisha ngozi.
  • Moisturizing — Kuipa ngozi unyevu na kuifanya iwe nyororo

Tuanze na Cleansing 

Cleasing ni kuosha uso wako na hapa unaweza kutumia cleanser hizi ni bidhaa ambazo zimetengenezwa viwandani kutumika kuoshea uso wako, unahitaji kujua una ngozi ya aina gani ili kupata ambayo inakufaa, lakini pia unaweza kuuosha tu kwa sabuni za kawaida, ukatumia vitu vya asili kama ndimu, limao au mtindi na kuosha uso wako.

Tunajua ngozi safi ni ngozi yenye furaha, ukiamka na kabla ya kulala inabidi uoshe uso wako, ili kuondoa mafuta, make up na jasho ambazo zinaweza kuharibu ngozi yako kwa chunusi au magonjwa ya ngozi, so first thing first hakikisha uso wako unakuwa msafi na ngozi yako kupumua.

Faida Za Kuosha Uso / Cleansing 

  • Hufanya ngozi kuwa yenye afya
  • Kusafisha husaidia bidhaa za kupambana na kuzeeka hufanya kazi vizuri

  • Husaidia ku-maintain proper pore size
  • Kusafisha kunahimiza proper skin hydration na kuzuia uzalishaji wa mafuta ya ziada.

Namna Ya Kuchagua Bidhaa Sahihi Ya Kutumia Kama Cleanser 

  • Jua aina ya  ngozi yako  na uchague cleanser ambayo ni mechi nzuri na ngozi yako. Ikiwa una ngozi kavu unatakiwa  kuepuka Cleanser ambayo ina high alcohol . Watu wenye ngozi ya mafuta huhitaji kusafisha  ngozi kwa kutumia cleanser zenye kiwango cha chini cha PH. Kwa ngozi sensitive unatakiwa kutumia basic cleanser free from heavy fragrance and additives.

  • Cream based cleansers ni nzuri kwa wenye ngozi kavu, wakati gel au foamy cleansers ni nzuri kwa wenye ngozi zenye mafuata

Muhimu pia kuuliza pale unapoenda kununua ni cleanser gani inafaa kwa ngozi yako.

Namna ya kufanya facial cleanser 

  • Paka cleanser kwenye viganja vyako na ufikiche /Warm your cleanser between your palm
  • massage cleanser yako katika uso wako, sugua uso kuanzia kwenye kidevu, mdomoni na karibu na machoni, usisahau kwenye shingo na masikio.
  • futa cleanser na kitambaa chenye unyevu
  • osha uso wako kwa kutumia maji ya vugu vugu.

Kwa leo tumejifunza kuhusu cleanser wakati ujao tunajua zaidi kuhusu Toning, tuambie je wewe una daily skin care routine yako ipoje?

Related posts

4 Comments

  1. a knockout post

    … [Trackback]

    […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine/ […]

  2. wavy bars

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine/ […]

  3. why not look here

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine/ […]

  4. Changa DMT For Sale Brisbane

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-kilasiku-skin-care-routine/ […]

Comments are closed.