Sasa hivi hata Dar es salaam sio ajabu kuona watu mbali mbali wamevalia makoti na majaketi kujiongezea joto la mwili kutokana na hali ya Baridi na upepo.
Mambo haya tulizoea kuyaona Arusha, Moshi na Maeneo mengine ndani ya Tanzania.
Ila sasa hali hii ipo Dar es Salaam na maeneo mengi, Ni vizuri ukajua nini ufanye ili ujiweke sawa wakati huu.
Changamoto kubwa ni baridi na upepo ambao unasababisha ukavu wa ngozi wa hali ya juu wengine inafikia hadi kukatika midomo na miguu na maeneo mengine.
Fanya yafuatayo kujiondolea ukavu wa ngozi.
- Kunywa Maji ya Kutosha.
Wakati huu sio sana kunywa maji kwa sababu ya hali ya hewa ila njia yenye matokeo chanya ni kujitahidi kunywa maji yako pia unaweza kuongeza limau au kununua maji yenye ladha tofauti.
- Usiende ukiwa na unyevu unyevu.
Hapa namaanisha, Kama ndio kwanza umetoka kupaka aidha lotion yako au mafuta yako subiri subiri kidogo ukitoka immediately baada tu ya kupaka, Ukipigwa na upepo utakauka zaidi.
- Tumia Products kutoka Vaseline.
Vaseline wanasifika kwa kutengeneza Products ambazo zinawafaa sana wenye ngozi kavu, wenye ngozi kavu sana. Wakati huu ngozi yako imebadilika sababu ya hali ya hewa na wewe badilisha vitu unayotumia.
- Kwa usoni ongezea Face oil.
Ukimaliza tu kupaka moisturizer yako paka face oil yako itafunga unyevu unyevu wako na hutahisi ukavu zaidi. Pia unaweza kutembelea ukurasa wetu huko instagram kujifunza zaidi kuhusu vitu vya kupaka kwenye ngozi yako.

- Wakati huu usifanye scrub zaidi ya Mara moja.
Wakati wa kipupwe kama hivi ngozi inapoteza unyevu kirahisi ukishindwa kuongeza bidii kwenye kumoisturize ngozi yako unaandaa mazingira mazuri ya ngozi kukauka na hutajiskia vizuri. Scrub kwa sasa fanya mara moja tu kwa wiki, usizidishe utasababisha ukavu zaidi.
Na baada ya kumaliza kufanya scrub yako Tumia Mask hapo hapo utaifanyia vizuri ngozi yako.
- Tumia hand Creams
Usiache mikono yako ikawa mikavu. Hakikisha unatumia hand cream.

- Kwenye lips tumia, Lip balm, lip jelly.
Tena ikibidi iwe portable uwe unaweza kuibeba kwenda nayo sehemu mbali mbali. Kwa wewe ambae una tabia lips zimekauka unarambisha mate wakati wa kipupwe na baridi haitakusaidia unaweza kupata vidonda.
Nilikwambia hapo juu usitoke nje ukiwa na unyevu unyevu subiri ukauke kwanza, kwa sababu ukipigwa na upepo utakauka zaidi ndio hivyo hivyo unarambisha mate kwenye lips ndivyo zinavyokauka zaidi. Nunua Lip balm.
- Vaa nguo zenye kukava mwili wako vizuri
ambazo wewe mvaaji utakuwa comfortable kufanya shughuli zako. Kumbuka unapojiacha wazi upepo ukikupiga utakauka zaidi. Fanya uchaguzi mzuri wa nguo zako.
- Pata muda mzuri wa kupumzika,
Na usiache kufanya night routine yako kwa sababu ngozi yako inajitengeneza vizuri usiku. Hasa wakati huu ambao inabidi ifanye kazi ya ziada kujilinda.
Tuambie wewe umekuwa unafanya nini wakati huu kuilinda ngozi yako na ukavu? Shea hapo chini kwenye comment!©️binturembo
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-yako-wakati-huu-wa-baridi-na-kipupwe/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-yako-wakati-huu-wa-baridi-na-kipupwe/ […]