SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kutunza Ngozi Yako Wakati Huu Wa COVD19
Skin Care

Jinsi Ya Kutunza Ngozi Yako Wakati Huu Wa COVD19 

Mlipuko wa ugonjwa wa Corona ( COVD 19) umeathiri Mataifa mbali mbali ikiwemo Tanzania. Hali hii imesababisha ratiba na mwenendo wa maisha kubadilika. Hapa chini tunakuletea jinsi unavyoweza kutunza ngozi yako wakati huu wa  COVD-19

  • Kaa mbali na Msongo wa Mawazo.Ugonjwa wa Corona upo, unatia hofu na ukifikiria sana unaweza kupata msongo wa mawazo na usijue cha kufanya na kuongeza hofu zaidi hii sio tu itaathiri kinga ya mwili wako bali hata afya ya ngozi yako na mwili kwa ujumla. Zuia vyanzo vyote vya msongo kama vile vyanzo vya taarifa zisizoaminika, anaekutumia ama wewe mwenyewe kwa kufatilia. Acha kufatilia vyanzo visivyoaminika kwa kuwa vitakuongezea hofu na mengine yatatokea yaliyotajwa hapo juu.
  • Fuata ushauri wa wataalamu kama wanavyosema na endelea kuchukua tahadhari. Afya tako ni muhimu, ukiwa na afya njema hio inahusisha na ngozi yako pia.
  • Vaa barakoa. Hii ni muhimu sana hasa unapotoka kwenda kwenye safari zako za lazima. Lakini ni muhimu sana kuvaa barakoa nusu saa baada ya kufanya skin care routine yako. Na usirudie kuvaa barakoa kama hujaifua / kuisafisha kwa zile zenye sifa ya kufuliwa. Ambazo hazina sifa hizo zitupe na kuziteketeza kama maelezo yanavyotolewa. Kurudia barakoa iliyo chafu sio tu itakuongezea shambulio la chunusi bali hata kukuweka kwenye hatari ya kupata maambukizi mengineyo. Usirudie Barakoa!
  • Nawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka na Sabuni.  Baada  ya kunawa paka hand cream/ hand lotion/ hand moiturizer/ hand oil kuzuia ukavu. Hizi zinaongeza unyevu kwenye ngozi, hasa kama wewe unapata ukavu baada ya kutumia moisturizer, paka hand cream yako ukavu utaondoka.
  • Changamoto ya skin care routine na barakoa.Kama una safari basi fanya routine yako nusu saa kabla ya kuvaa barakoa na usirudie kuvaa barakoa.
  • Jitahidi kuwa off make up kuzuia congestion ya materials kwenye ngozi yako. Ufanye routine yako upake make up kisha uvae barakoa unaweza kuona ni jinsi gani inaweza kuwa changamoto kwako. Chagua kuwa off make up. Kama ni lazima kupaka make up, tumia original products na utakaporejea osha make up yako kabla ya kulala na ukumbuke kufanya skin care riutine yako ya usiku. Na ile barakoa yako ioshe pia na kama ni ya kutupa itupe kama inavyotakiwa ama kuichoma moto.
  • Barakoa za kufua, fua kabla ya kuzivaa tena. Na upige pasi kuhakikisha unaua wadudu mbali mbali ambao si tu wataathiri afya ya ngozi yako hadi afya yako kwa ujumla.
  • Kama si lazima kutoka nje ya nyumba yako baki nyumbani na uendelee kuwa salama kutokana na hali ya huko nje pamoja na jua. Kama kuna ulazima wa kutoka nje ya nyumba yako, Chukua tahadhari ya kuepuka mikusanyiko, kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono, kuepuka kukaa karibu na watu na kutumia vitakasa mikono ” sanitizer”.
  • Usiache kutumia sunscreen. Sunscreen ni muhimu sana, uwe unaenda nje, au hauendi uwe unatoka au hutoki. Endelea kufanya skin care routine yako kama kawaida na Usiache kutumia sunscreen.

Jilinde na uwalinde wengine, Baki Nyumbani ubaki salama.

Jee wewe unafanya nini zaidi kuendelea kuwa na ngozi yenye afya wakati huu wa COVD 19 ?

Shea na sisi kwenye comment!

©️binturembo

Related posts

4 Comments

  1. weed delivery toronto

    … [Trackback]

    […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-yako-wakati-huu-wa-covd19/ […]

  2. all slot auto wallet

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-yako-wakati-huu-wa-covd19/ […]

  3. Blue meanie magic mushroom

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-yako-wakati-huu-wa-covd19/ […]

  4. golden teacher mushroom feeling,

    … [Trackback]

    […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kutunza-ngozi-yako-wakati-huu-wa-covd19/ […]

Comments are closed.