SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kuwa Na Ngozi Nyororo
Urembo

Jinsi Ya Kuwa Na Ngozi Nyororo 

Hatuwezi kukataa sote tunahitaji ngozi laini na nyororo, lakini mbinu au njia tunazotumia muda mwingine hutuacha na matokeo tusiotaraji kupata baada ya kufuata njia hizo. Ni kwasababu tumeumbwa tofauti na tunadhani kutumia njia iliyomsaidia mwingine itatusaidia na sisi na kugundua ni kinyume kabisa. Usijali, hizi hapa njia nane za kufuata ambazo zitakusaidia haijalishi ni aina gani ya ngozi ulionayo.

1. ULAJI (MLO)

fruits and vegetables Utashangazwa kujua kuwa vitu unavyokula vilivyokuwa na mchango mkubwa katika ngozi na afya yako kwa ujumla. Ilikupata ngozi nzuri, laini, nyororo na inayong’aa inabidi kuacha vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa viwandani, wanga, mafuta na sukari na badala yake kula protini, matunda, mbogamboga na maji kwa wingi. Hakikisha unakunywa maji sio chini ya glasi 8 kwa siku  na matunda pamoja na mbogamboga kila unapopata mlo. Matunda na mbogamboga husaidia oxygen kuzunguka vizuri mwili na kwenye ngozi kuliko mafuta au kipodozi chochote unachoweza kupaka. Protini unasaidia kujenga ulinzi zaidi katika seli za ngozi ambayo ngozi inahitaji kukabiliana na ukavu wa ngozi. Na maji husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini na kusaidia vitundu vya ngozi kupumua vizuri, hivyo kuzuia bacteria wanaojificha chini ya ngozi.


2. MUDA WA KUPUMZIKA 
Watu wengi hawatambui umuhimu wa usingizi katika kutunza ngozi na kuzuia kuzeeka haraka. Usingizi ni muhimu kwa ngozi yako sana, hakikisha unapata muda wa kutosha kulala usiopungua masaa 8. Kifiziolojia, ngozi inafanya kazi kubwa sana wakati wa mchana katika kutunza mwili, kukabiliana na mionzi ya jua, kukabiliana na vijidudu mbalimbali kama bacteria na virusi na kutizamia joto la mwili. Ngozi hujijenga wakati mwili umepumzika ili kuweza kuendelea kuchunga mwili wa mwanadamu ipasavyo. 


3. ACHA KABISA KUJITUMBUA.
Kutumbua chunusi na vipele ni tabia tulionayo wengi ambayao husababisha makovu, wekundu na kusambaza bacteria (hupelekea matatizo zaidi ya ngozi) kwenye maeneo ya ngozi ambayo hayana matatizo. Japokuwa ni ngumu kutotumbua mchunusi unaokutazama, ikibidi bora kutumia vitambaa kisafi kutoa chunusi na sio vidole au kucha kwasababu ya uchafu uliopo kwenye kucha na vidole waweza kusambaza maambukizi katika maeneo mengine ya ngozi, japo ni vizuri na inashauriwa kumuona mtaalamu wa ngozi ili akupatie tiba ya uhakika.


4. USAFI KWANZA.
Osha uso wako kwa maana ya kuosha sio utani. Watu wengi hukimbilia kuosha nyuso zao harakaharaka na sio vizuri kusafisha uso juujuu kwasababu kuna uwezekano mkubwa wa uchafu kubaki, msichana unatakiwa kutambua umuhimu wa uso wako na kutenga muda wa kutosha katika kuosha na kutunza  uso wako . Chukulia kuosha kikaangio chenye mafuta na kukiosha juujuu , kama hutochukua muda wako kuosha na kusafisha mafuta yatabakia kwenye kikaangio, vivyohivyo inavyokuwa katika uso wako. Hivyo kusafisha uso mara zisiopungua mbili kwa siku ni vizuri kwa utunzaji wa ngozi yako ya uso na kupaka mafuta baada hajilishi ngozi yako ina mafuta au inamafuta. Mafuta ni kwaajili ya kulainisha na kung’arisha ngozi hata kama una ngozi ya mafuta mengi  ni vizuri kutafuta mafuta ya ngozi yako (oily skin)


5. JALI MACHO YAKO.
Watu wengi wetu hupaka kiasi kidogo cha mafuta chini ya macho bila kujua faida tunazoziacha kwa kutokufanya hivyo. Tabasamu  — kisha angalia kwenye kioo. Kuna mistari(mkunjo) ambayo inaanzia kwenye jicho, amabyo muda mwingine husogea hadi kwenye maeneo ya karibu na nywele. Paka mafuta ya kutosha chini ya macho fanya kama kumassage flani hivi kwanzia kwenye kona karibu na pua mpaka kwenye mfupa wa shavuni(cheekbone) kuzunguka jicho lote. Fikiria lile eneo linalofunikwa na miwani na upake mafuta ya kutosha kuzunguka eneo hilo.


6. BARAFU
Barafu?! Inashangaza, najua ila moja kati ya vitu licha ya upatikanaji rahisi ni uwezo wake wa kutunza ngozi yako bila gharama. Kati  faida za kutumia barafu katika utunzaji wa ngozi yako ni; Ukiumia au kujichuna kwenye ngozi waweza kutumia barafu kupunguza wekundu na kuwaka moto katika eneo lile, sote tunajua unapochubuka au kuumia kuna hali ya moto ambayo tunapata katika eneo lile tumia barafu itakusaidia. Pia barafu unaweza kutumia kupunguza ukubwa wa matundu katika ngozi hasa pale mtu alipokuwa amekamua chunusi, barafu husaidia kuvuta ngozi ilisiwe imeacha matundu ambayo muda mwingine hayapendezi kuonekana. Ila kumbuka wakati wa kutumia barafu zungusha maeneo tofauti kwasababu huunguza pale inapoachwa sehemu moja. Pia ni vizuri kuweka aloevera katika maji utakayo gandisha kwaajili ya barafu (hiari yako)


7. TUMIA MAFUTA HUSUSANI KWA AJILI YA NGOZI.
Moja kati ya njia za kutapa ngozi laini na nyororo ni kutumia mafuta ambayo yametengeneza kwaajili ya kupaka kwenye ngozi na sio ya nywele au ya kula. Kutumia mafuta ya ngozi yanang’arisha ngozi na muonekano mzuri ambao sio wa mafuta. Mafuta ya ngozi hayazibi vitundu vya ngozi hivyo huruhusu ngozi kupumua na kutoa taka mwili kupitia vitundu hivyo na yana saidia kupunguza uzajishaji wa mafuta katika uso hasahasa kwa wale wenye ngozi za mafuta. Kumbuka kupaka mafuta mara mbili kwa siku katika uso msafi yani baada ya kusafisha uso vizuri ndo upake mafuta na utaona mabadiliko katika ngozi yako, mabadiliko mazuri!


8. ULINZI BINAFSI
Kwa wale wenye matatizo ya kuung’ua na jua asubuhi paka mafuta ya kuzuia mionzi ya jua (sunscreen)inayopenya kwenye ngozi na kuharibu ngozi yako. Na pale unapokuwa nje hakikisha unajizuia na jua kwanzia mavazi yako, vaa miwani za kuzuia jua na kofia pana inayozuia jua kupiga usoni.

By @binturembo

Related posts

5 Comments

 1. look at more info

  … [Trackback]

  […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuwa-na-ngozi-nyororo/ […]

 2. smiley drogen,

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuwa-na-ngozi-nyororo/ […]

 3. furbabiescavoodlepuppies

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuwa-na-ngozi-nyororo/ […]

 4. Dark web market links

  … [Trackback]

  […] There you will find 7158 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuwa-na-ngozi-nyororo/ […]

 5. 토렌트 사이트

  … [Trackback]

  […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/jinsi-ya-kuwa-na-ngozi-nyororo/ […]

Comments are closed.