SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

JIONGEZE KUJUA KIUNDANI KUHUSU LIPSTICK
Urembo

JIONGEZE KUJUA KIUNDANI KUHUSU LIPSTICK 

Lipstick ni kipodozi chenye rangi ambacho mara nyingi upakwa mdomoni na ipo katika muundo wa kimti (lip-mdomo, stick-mti).

Lipstick zipo za aina na rangi na zina faida tofauti tofauti kwanza tutaanza na aina za lipstick,

Lipstick kavu – hizi hazina mafuta kabisa ukipaka zina kaa kwa muda mrefu sana na pia hufanya upate muonekano natural na bold. kwa sasa ndizo hutumika sana

Color-Sensational-The-Creamy-Mattes

Lipstick za mafuta – hizi ni zile zenye mafuta hazichukui muda kufutika, lakini ni nzuri kwa ngozi ya midomo yako hasa kwa wale wenye midomo mikavu husaidia kuto kubabusha ngozi. Kwa sababu hizi ndizo zilikua za kwanza kabla ya kavu ndani yake kuna aina mbali mbali za lipstick lakini zote kwa ujumla uitwa lipstick za mafuta.

AuxiliaryIOTWPrettyZombie

Faida za Lipstick kuna faida mbali mbali za kupaka lipstick baadhi yake ni:

uzuri- lipstick zinakupa muonekano mzuri usoni, ukiwa umepaka lipstick ya rangi yoyote ile ina kuongezea uzuri wako katika uso pia kama una hitaji kusimama mbele za watu au una hitaji kujiongezea kujiamini basi Lipstick ndio jibu lako.

Kuipa midomo yako unyevu – kutokana na kuwa na mafuta na baadhi ya kemikali zenye mafuta na afya Lipstick zina saidia kuipa midomo yako unyevu ambao husaidia kuto kuharibika kwa midomo yako (mf; kubabuka midomo).

Jua – midomo ipo usoni kuikinga na jua ni kazi sana ni hadi uvae kofia lakini ni vipi endapo sehemu unazo tembelea mara kwa mara hazikuruhusu wewe kuvaa kofia? ni vyema ukapaka lipstick ili kuzuia midomo yako kuharibika na jua, baridi au hata upepo ambapo vitu hivi vinaweza kuiletea midomo yako madhara.

lipstick zina kemikali mbali mbali ambazo zinaweza kusaidia kuikinga midomo yako na baadhi ya magonjwa.

Namna nyingine ya kutumia Lipstick

japo ime zoeleka lipstick hutumika katika midomo tu kuna namna nyingine ambapo lipstick ina weza kukusaidia

1) kuifanya kuwa highlighter

MTIzMDQ5NjY1MjQzNDgxNjEy

inaweza ikawa umesahau kubeba highlighter yako lakini kwenye pochi una lipstick yenye rangi ya highlighter labda rangi ya brown, unaweza kuitumia kama highlighter na ika kupa matokeo mazuri.

2)Lipstick kama eyeshadow

woman-red-eyeshadow

pia una weza kutumia lipstick kama eyeshadow na ika pendeza tu aina yoyote ya lipstick ina pendeza kuwa kama eyeshadow iwe lipstick kavu au ya mafuta lakini ni vizuri pia ukatumia zile rangi za kuonekana zaidi kama nyekundu, blue nk.

3) Lipstick kama tattoo

woman-with-bird-tattoos-on-forearm

inaweza ikawa una penda tattoo lakini hupendi kuchora, unaweza kutumia Lipstick kwa kujichora vizuri kama tattoo na baadae ukatoa

 

 

Related posts

2 Comments

  1. magic mushrooms blue meanies

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/jiongeze-kujua-kiundani-kuhusu-lipstick/ […]

  2. visit

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/jiongeze-kujua-kiundani-kuhusu-lipstick/ […]

Leave a Reply