SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jua Nini Unachosema Kwa Namna Unavyobeba Mkoba Wako
Urembo

Jua Nini Unachosema Kwa Namna Unavyobeba Mkoba Wako 

Kwa wanawake kutembea na mkoba ni kitu cha kawaida, kwa wao kuhifadhia vitu vyao lakini pia ni moja ya urembo ambao unapendezesha mitoko yao, lakini inawezekana wasijue au usijue kwamba kuna kitu unazungumza kwa jinsi au namna unavyobeba mkoba wako, well tumetafuta zile common ways ambazo tunaona wanawake wengi wanabeba mikoba yao na huwa wanazungumza nini wakibeba mkoba kwa namna hio.

 

 • Mkoba ukiwa umebebwa kwapani wakati umefunga mkono/mkoba ukiwa karibu na mwili

Kwa sasa hivi wengi wanao beba hizi mkoba ni wakina mama, wadada wengi sasa hivi hawabebi hivi mkoba lakini kama wewe ni mmoja wa watu ambao unabeba hivi mkoba maana yako ni kwamba wewe ni mtu wa kuaminika, mtu ambae unapenda kufanya vitu vikakamilika na hupendi kupoteza muda wako katika vitu vidogo visivyo na maana. Lakini pia inaamika kama ukiwa umebeba mkoba wako hivi na umeushikilia kwa nguvu kidogo wewe ni mtu mwenye uoga, lakini inawezekana pia unahofu ya kuibiwa.

Lakini kama utabeba kwa namna hio huku mkoba wako ukiwa una ning’inia freely basi wewe ni mtu ambae upo carefree na unachukulia maisha vile yalivyo, lakini pia ni mtu ambae unapenda uhuru wako na sio kubanwa banwa na unaujasiri pia.

 • ukibeba mkoba katika kiwiko cha mkono 

Hivi ndivyo wadada wengi wanabeba handbags siku hizi kama wewe ni mmoja wapo basi unaonyesha kwamba unapenda ufahari na mamlaka, unaweka kipaumbele katika nyadhifa lakini pia wakati mwingine unaweza kuonekana kama “highly maintanace” na  unajua unayotarajia kupokea kutoka ulimwenguni. Watu maarufu wengi hupenda kubeba mikoba yao kwa namna hii wengine ni kutokana na ukuwa wa mkoba hawataki kuonekana umewazidi lakini pia kuonyesha brand ya mkoba huo. 

 • Kubeba Mkoba Mkononi

Kuna wale ambao hupenda kubeba mkoba wao kwenye kiganja kama wamebeba ndoo ya maji, kuna mikoba mingine ambayo ni midogo sana unakosa chaguo la kubeba zaidi ya kubeba hivyo lakini pia kama utakuta mwanamke ana beba mkoba wake hivi basi jua kwamba anaonyesha jamii yeye ni zaidi ya mwanamke wanae mfikiria na anaonyesha umuhimu wake katika kazi, wengi huwa wanabeba briefcase namna hii.

 

 

Related posts

2 Comments

 1. youtube video download

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/jua-nini-unachosema-kwa-namna-unavyobeba-mkoba-wako/ […]

 2. Buy Unprescribe DMT Online

  … [Trackback]

  […] There you can find 33112 additional Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/jua-nini-unachosema-kwa-namna-unavyobeba-mkoba-wako/ […]

Comments are closed.