SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jua Toauti Ya Vipodozi Organic Na Natural
Dondoo

Jua Toauti Ya Vipodozi Organic Na Natural 

Kila asubuhi wanawake wengi yumkini na wewe unaesoma hapa unaweza kuwa mmoja wao huamka na kupaka vitu tofauti tofauti mwilini. Kile ambacho wengine hawaachi kufikiria ni nini wanaweka kwenye ngozi yao.  Vipodozi vingi sana na bidhaa za utunzaji wa ngozi leo zimejaa viambata vyenye kemikali zenye kuharibu afya. Vingine hadi  vimehusishwa na kansa.

Hadi sasa ongezeko la uhitaji na utolewaji wa elimu kuhusu vipodozi na ubora wake umeongezeka na kila mwanamke hata wewe unaesoma sasa hivi unatamani vipodozi natural. Baada ya kumaliza kusoma makala hii leo utaweza kujua Tofauti ya natural na organic na kati ya hizo ipi ni bora zaidi kuliko nyengine!


Tofauti kati ya kipodozi organic na kipodozi natural. Kwa haraka haraka unaweza ona kama ni kitu kile kile. Ila ukweli ni kwamba sio kila natural ni organic. 


Kivipi? 


Ili bidhaa iwe organic inatakiwa viambata vyake vitoke kwenye mashamba yanayolimwa bila mbolea za viwandani maana mbolea hizo huwa na kemikali. Kwa hio hufanya hivyo viambata visiwe organic. 
Imekuja trendy watu wanasema wao wanatumia organic. Huku wakisahau kua yumkini nazi unayotengenezea mafuta nyumbani imeoteshwa na mbegu za kisasa au imewekwa mbolea ya kiwandani. Kwa maana nyingine  ni kua natural peke yake haitoshi, Inatakiwa  iwe organic ili iwe salama zaidi.


Bidhaa  nyingi ambazo ni natural tunaziita natural kwakua hazina paraben kama kihifadhia bidhaa isiharibike (preservative) pia bidhaa inaitwa natural kwa sababu imetengenezwa na mimea na haijafanyiwa  majaribio kwa panya. 


Ila ukisikia na kuona kipodozi organic ujue hicho kimetengenezwa na malighafi ambazo toka shambani na chanzo chake hazijaongezewa chochote vile vile hazijawekwa kihifadhia bidhaa isiharibike. Ndio kusema Organic ni bora zaidi ya Natural kwa usalama wa matumizi yako.


Kwa upande wa bei na gharama organic ni bei au tuseme gharama  yake iko juu zaidi ya ile natural, Natural bei au gharama yake ni nafuu kiasi japokuwa zote ni affordable inategemea na  mhusika.
Baada ya kuelewa tofauti hizo, Hivyo basi utaamua mwenyewe kwa wewe ni bora organic au Natural!
Je wewe unatumia zaidi natural or Organic?

©️binturembo

Related posts

1 Comment

  1. polka dot psilocybin chocolate bar

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/jua-toauti-ya-vipodozi-organic-na-natural/ […]

Comments are closed.