SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jua Zaidi kuhusu Kutengeneza Cream Nyumbani
Skin Care

Jua Zaidi kuhusu Kutengeneza Cream Nyumbani 

Najua hapo ulipo unawaza na kufikiri je ni kweli nitaweza kutengeneza cream ya uso nyumbani kwangu na ikafanya kazi?
Kabla ya kujibu swali hilo nataka usome hadi mwisho kisha utajua kama ukitengeneza itafanya kazi au lah!


Kutengeneza cream nyumbani kwako ni njia nzuri ya kupunguza matumizi na kujiaminisha  kwamba nitapata kitu natural hivyo nitaepukana na sumu za vipodozi vya madukani  na gharama ya vipodozi.


Vile vile ni njia nzuri ya kutengeneza bomu ambalo hujui litakuripukia muda gani!


Usishtuke, bado nasisitiza usome hadi mwisho ili uweze kuelewa jee ni kweli cream utakayoitengeneza itafanya kazi!
Ili uweze kutengeneza cream na ifanye kazi unatakiwa kujua yafuatayo

:✔️Uwe unajua ni nini na nini kinaweza kuchanganywa bila ya kuharibu formula ya kitu husika na kwa kiasi gani!

✔️ Uwe unajua mazingira sahihi ya kutengeneza kitu husika. Unajua kwamba kemikali zingine huharibika tu zinapopata mwanga wa jua, au upepo?

✔️Uwe unajua namna sahihi ya kuzihifadhi mara tu unapomaliza kutengeza!

✔️Uwe unajua ni vimiminika gani vinahitajika katika kuchanganyia vitu husika, Jee unajua unatakiwa kutumia maji fresh au maji distilled ? Hii ni kwa sababu maji ya bomba bado sio pure kuweza kuchanganya na kutengeneza mchanganyiko ambao utataka udumu kwa muda kidogo, baada ya masaa machache huwa imeharibika na badala ya kupaka kitu salama unapaka bomu ulilitengeneza mwenyewe katika ngozi yako nzuri ya asili


Sio hayo tu, kuna mengine mengi ili kuhakikisha kitu bora kinagusa ngozi yako!
Sisi kama afroswagga tunakushauri kama unania, wazo ama unafanya mtindo huu acha mara moja kwa sababu madhara mengi yanayotokea kwenye ngozi yako leo sio matokeo ya kitu ulichokifanya jana ni masiku mengi huko nyuma.
Hapa tunamaanisha, Ukianza kufanya hivyo leo madhara yake huja kuonekana baada ya miaka kupita!


Kama unapenda home remedies

✔️Hakikisha  unatengeza batch ndogo ndogo, unatumia unamaliza!✔️Unachanganya vinavyochanganyika kwa kufuata maelekezo husika.

✔️Ni bora zaidi kutumia remedy moja kama ilivyo zingine zinajitosheleza!✔️Na ni ukweli usiopingika huwezi Ku DIY kila kitu kwa usalama wa ngozi yako, vingine andaa bajet yako na ununue kutoka kwa genuine brand mana zipo kwa affordability ya kila mmoja!


Kingine, mara nyingi hizi home made cream hazinaga label, wala description zinazoonesha kilichotumika na kiasi chake, expire date wala siku iliyotengenezwa sijui unajihakikishiaje usalama wa kipodozi husika!
Ngozi yako ni nzuri sana hakikisha unachukua tahadhari katika kile kinachokuja karibu yako! Najua una hamu ya kutatua tatizo lako, lakini usalama wako ni muhimu zaidi usizidishe tatizo!
Jee hadi sasa utatengeneza face cream nyumbani?
©️binturembo

Related posts

3 Comments

 1. Lyophilized Goldmember Magic Mushrooms

  … [Trackback]

  […] Here you will find 43979 additional Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/jua-zaidi-kuhusu-kutengeneza-cream-nyumbani/ […]

 2. Check This Out

  … [Trackback]

  […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/jua-zaidi-kuhusu-kutengeneza-cream-nyumbani/ […]

 3. Buy Albino Penis Envy Mushrooms For sale Canbera

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/jua-zaidi-kuhusu-kutengeneza-cream-nyumbani/ […]

Comments are closed.