Wenzetu wanaviita wicker basket bags sisi tunaita Kikapu/Vikapu, hivi hutengenezwa na majani ya milulu ambayo pia hutumika kutengenezea mikeka, kwa hapa kwetu Tanzania vinapatikana sana maeneo ya Iringa japo hata nikoa mingine pia vipo.
Huku kwetu mabibi ndio wanavibeba sana na hutumika kwendea sokoni lakini kwa wenzetu wao wana beba kama handbags na wana vistyle hasa mpaka unasahau kama kile ni kikapu. Tumeona huko kwa wenzetu na tukaona tuwaletee hapa tupate kujifunza namna ya kutumia vitu vyetu kisasa zaidi, baadhi ya fashionista’s kutoka Nje Ya Nchi wameonekana kuvutiwa na hivi vikapu na wengi wanasema wanavipenda kwa maana vinabebeka na kuvalika na kila aina ya vazi
Wao wameboresha kidogo kwa kuweka kila aina ya size lakini pia wametengeneza vya aina tofauti tofauti.
Pia wameongezea na urembo mwingine kama pom pom’s, leather na vingine vingi
Kwa hapa Tanzania tumemuona stylist Joujou Nyaki akiwa amebeba Kikapu kama Kipochi
kama umependa style hii na unatafuta wapi pa kuvipata masokoni huwa wanauza sana lakini pia kama unataka designer made kikapu yupo mbunifu kutoka Tanzania Doreen Mashika anavitengeneza
Tuambie je Umependa kikapu handbag au vibaki tu kuwa vya kubebea nyanya sokoni?
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/kikapu-kinavyo-tumika-kama-handbag/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/kikapu-kinavyo-tumika-kama-handbag/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/kikapu-kinavyo-tumika-kama-handbag/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/kikapu-kinavyo-tumika-kama-handbag/ […]