SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Kung’ata Kucha Hupoteza Haiba Ya Urembo Wako
Urembo

Kung’ata Kucha Hupoteza Haiba Ya Urembo Wako 

Ingawa inawezekana wengine wakaona kitu cha ajabu, lakini ukweli ni kwamba kukata kucha kwa meno ni jambo linalofanywa na watu wengi.

Ni wazi kuwa si muda wote utakuwa na uhakika kuwa mikono yako ni safi na salama, hivyo inaweza kusababisha kujitafutia magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika.


Kwenye upande mzima wa urembo, mtu anayeng’ata kucha anapoteza sifa yote ya kuitwa mrembo kutokana na kitendo hicho kuhusishwa na uchafu.
Wapo wanaofanya kwa makusudi na wengine hujikuta waking’ata vidole na kukata kucha bila kujitambua kama wanafanya kitendo hicho.
Mara nyingi hali ya kukata kucha bila kujitambua inatokana na mazoea ambayo mtu amejijengea hasa anapokuwa amezubaa na kukosa kitu cha kufanya hivyo kujikuta mikono yake ikielekea mdomoni.


Japokuwa wengi tunaamini mikono yetu, lakini kiafya kukata kucha kwa kutumia meno kunaweza kuleta madhara kadhaa ikiwamo kubeba vijidudu na kuviingiza mdomoni.
Bila kujitambua unaweza kujikuta ukivichukua vijidudu vinavyojificha kwenye kucha na kuvipeleka kwenye mdomo jambo ambalo linaweza kusababisha hatari


Hiki kitu kina waathirika wengi sana wake kwa wanaume wakubwa kwa wadogo. Tunaweza kudhani tu kuwa ni tabia mbaya au mazoea! La hasha kutafuna kucha za vidole vya mikononi ni tatizo la kisaikolojia linalomla mtu ndani kwa ndani kwenye ufahamu wake ambapo hupelekea viashiria hivi:-
-woga-mawazo/msongo wa mawazo-kutojiamini-fadhaa/sononi-kukosa la kufanya-taharuki-mapepe/restless mind-hulka ya kuiga 
Hivyo ni viashiria vikuu vya mtafuna kucha na hili jambo hufanya bila kupenda ni involuntary action. Kuna baadhi hufanya wakiwa pekeyao kwenye upweke na wengine hufanya pindi anapokutana na mtu kwa mara ya kwanza ama hadhira.


Kwakuwa hili ni tatizo la kisaikolojia zaidi basi hata tiba yake ni ya kisaikolojia, hasa hasa 
-councelling/ushauri nasaha-

kumjengea uwezo wa kujiamini mwathirika

-kutafiti kupitia yeye mwenyewe chanzo cha tatizo lake hilo na muda 
Wengine hukutana na hii hali katika hatua fulani ya makuzi na ikipita tatizo hujitibu lenyewe!


Je una tatizo kama hili ama ndugu yako? Ama rafiki? Usikimbilie kwa mganga wa kienyeji utaambiwa una jini njaa..! Tiba unayo mwenye
©binturembo 

Related posts

5 Comments

 1. magic mushroom chocolate bar packaging

  … [Trackback]

  […] Here you can find 76888 additional Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/kungata-kucha-hupoteza-haiba-ya-urembo-wako/ […]

 2. Best magic mushroom shop Australia

  … [Trackback]

  […] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/kungata-kucha-hupoteza-haiba-ya-urembo-wako/ […]

 3. read here

  … [Trackback]

  […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/kungata-kucha-hupoteza-haiba-ya-urembo-wako/ […]

 4. Oxandrolon Erfahrung

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/kungata-kucha-hupoteza-haiba-ya-urembo-wako/ […]

 5. liquid cannabis for sale

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/kungata-kucha-hupoteza-haiba-ya-urembo-wako/ […]

Comments are closed.