SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Kunywa Kinywaji Hiki Kupata Ngozi Yenye Mvuto
Urembo

Kunywa Kinywaji Hiki Kupata Ngozi Yenye Mvuto 

Kupaka vipodozi pekee hakuwezi kukupa ngozi nzuri, bali pia unahitajika kuangalia unachokula pamoja na life style yako, ikiwa kuna hitilafu kwenye kimoja wapo basi utatumia nguvu nyingi sana kupata ngozi unayoitaka.

Ikiwa moja ya vitu ambavyo tunashauriwa kula kwaajili ya ngozi nzuri ni matunda na mbogamboga , inawezekana wewe si mpenzi wa vitu hivi basi unaweza kutengeneza juice ukanywa.

Moja ya juice ambayo inatajwa kuwa inafanya kazi vyema kwenye ngozi ni Juice ya carrot na manjano, je vinasaidiaje katika ngozi?

  • Mizizi Ya Manjano / Manjano Mbichi

hufanya kazi kama moisturizer ya asili katika ngozi ambayo inaweza kusaidia kufanya ngozi kuwa laini na nyororo na kuzuia ngozi kuwa kavu. Ina anti-fungal, antibacterial na anti-inflammatory properties, yote ambayo zinamanufaa manufaa kwa watu wenye chunusi.

Inasaidia kukupa youthful skin na kupunguza kasi na dalili za kuzeeka na pia inaweza kusaidia kuzuia ngozi isizeeke mapema. Kwa wale walio na rangi tofauti mwilini, kunywa maji ya manjano kunaweza kusaidia kupunguza kuonekana kwa mabaka meusi kwenye ngozi na kuzuia ngozi kuwa nyeusi.

  • Carrot

Carrot ina compound iitwayo beta carotene ambayo inaweza kusaidia kuimarisha afya ya ngozi. inaweza kusaidia kulinda ngozi dhidi ya miale ya UV (jua) na pia inaweza kusaidia kupunguza uharibifu wa ngozi na kuboresha mwonekano wake kwa ujumla. Ina vitamini V kwa wingi na ina antioxidants inavyoweza kusaidia kutengeneza tishu za ngozi zilizoharibika, huku pia ikisaidia kuboresha na kuipa mng’ao ngozi.

  • Amla / Indian Gooseberry

Amla ina kiwango cha juu cha antioxidants ambayo inaweza kusaidia kuchelewesha dalili za kuzeeka kama mikunjo ya uzee na fine lines pia inaweza kuzuia kuzeeka mapema kwa seli za ngozi. Inaweza pia kusaidia kupunguza weusi katika ngozi.

Inaweza pia kusaidia kuboresha rangi, umbile,mwonekano wa ngozi, na hivyo kukupa mng’ao bora wa ngozi na mwonekano mzuri.

Viungo

  • Carrot
  • Manjano Mbichi
  • Amla / Indian Gooseberry
  • Maji

Namna Ya Kufanya

Osha karoti, mizizi ya manjano na amla kwa maji sadi ili kuondoa uchafu. Unaweza pia kuzilowesha kwa maji kwa nusu saa kabla ya kuzitumia.

Kata karoti na amla vipande vipande na uweke kwenye bakuli.

menya / toa ngozi manjano na ukate vipande vipande na uweke kando.

Weka karoti, manjano mbichi na amla pamoja na maji na uchanganye kwenye blender na u-brend mpaka vikiwa laini.

chuja na unywe unaweza kuweka kwenye fridge na ukainywa ikiwa ya baridi.

Related posts