SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Kutokulala Vyema Kunavyo Athiri Ngozi Yako
Urembo

Kutokulala Vyema Kunavyo Athiri Ngozi Yako 

Wakati uko busy ku-keep up na night life, kwenda club, kuangalia movies / series usiku kucha ndivyo ambavyo unaharibu ngozi yako pia bila ya kujua, ushauri wa wataalamu wa ngozi ni kulala kwa masaa 7 hadi 8, kulala vyema kunasaidia kupata ngozi nzuri lakini pia utajiuliza ni nini kitatokea endapo hutolala kwa masaa hayo tajwa?

Well tunakuletea ni nini kitatokea endapo utakosa kulala vyema

  • Ngozi Yako Kutokuwa Sawa (Imbalanced)

Kuto kupata usingizi wa kutosha kutafanya ngozi yako kutokuwa sawa, utaonekana na utaonekana dull, unapokosa usingizi wa kutosha unaweza kusababisha upungufu wa PH levels katika ngozi yako na kufanya ngozi ikose rangi sawa kuonekana dhaifu pia ngozi kuwa kavu.

Unaweza ukawa una kunywa maji ya kutosha na kutumia product sahihi lakini ngozi bado ikawa haijakaa vyema na hii ni kutokana na kutokulala vya kutosha.

  • Ngozi Kukosa Nuru

Wote tunapenda tuwe na ngozi yenye nuru wenyewe tunaita ku-glow, kuipata hii ngozi sio tu kupaka skincare routine na sun screen bali pia kufuatisha vitu muhimu kama kulala vyema, unapokosa usingizi wa kutosha cortisol level zinaongezeka ( homoni zinazohusiana na stress) na kusababisha Inflammation ambazo zinaweza kusababisha protin zilizopo katika ngozi yako kushuka na kupelekeanukosaji wa nuru katika ngozi

  • Kupata Chunusi

kama tulivoelezea mwanzoni Usipopata usingizi wa kutosha, homoni zako za msongo wa mawazo huongezeka na hiyo ina maana hivyo ndivyo uwezekano wa kupata chunusi. Sio hivyo tu bali viwango vya cortisol vilivyoongezeka pia ni kiashiria cha kuongezeka kwa uzalishaji wa mafuta na sote tunajua kwamba hii inaweza kusababisha pores kuziba na pimples zisizohitajika na madhara mengine ya ngozi.

  • Kupata Mikunjo Ya Uzee

kuongeza viwango vya cortisol kuna uhusiano wa moja kwa moja na uzalishaji wa pf collagen (protini inayoathiri unyumbufu wa ngozi yako na kukabiliana na kuzeeka kwa ngozi yako). Uzalishaji huu wa collagen unapoongezeka kwa sababu ya ukosefu wa usingizi, ngozi yako inaweza kuwa nyembamba, kutokuwa firm nakukosa kuwa smooth. Hii inamaanisha kuwa uso utaanza kuonekana na makunyanzi kabla haijatakiwa, na jamani, tunajua kuzeeka sivyo ilivyokuwa zamani sasa hivi kila mmoja wetu anapenda kuonekana under 18

Je unawezaje kuondokana na yote haya? Fanya skincare, kunywa maji yatosha, epuka stress,paka sunscreen na kikubwa LALA VYA KUTOSHA

Related posts