SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Kwanini Uwekezaji Katika Urembo Tanzania Unazorota?
Urembo

Kwanini Uwekezaji Katika Urembo Tanzania Unazorota? 

Wakati wenzetu wakiendelea ku-invest katika urembo sisi kwetu kuna zidi kuzorota, kama ni mfanya biashara utakubaliana na sisi kwamba sasa hivi wafanya biashara wa fashion na vitu vya urembo ndio wanao uza zaidi, wanawake kwa wanaume wana penda kuonekana smart kwa sasa kuanzia nywele, mavazi,viatu, kucha, accessories na hata mikoba.

Tukiangalia kwa wenzetu watu maarufu mbali mbali wana jikita katika sekta hizi kwa mfano Muimbaji Rihanna ukiachana na collaboration zake na wabunifu ana kampuni yake ya urembo ya Fenty Beauty, Kim Kardashia ana KKW, Kylie Jenner ana Kylie Lip Kit na sasa tuna sikia mwanadada Serena Williams anataka kuja na brand yake ya urembo pia. Hii ikatufanya tuwaze kwanini kwetu hatuwekezi? na hata tukiwekeza havifiki mbali?

Achana na T-shirts ambazo wasanii na watu maarufu wetu wengi walijaribu kufanya, turudi katika urembo tumeona watu mbali mbali wakijaribu kuingia huku na kutoka pangu patupu japo ambao kuna wale ambao wame maintain mpaka leo, mfano Shekha Manjano, Shekha ana miaka minne katika biashara hii japo si wengi wanajua ni product ya Tanzania lakini bora ya yeye ame weza kuendelea kukaa katika soko hili kwa muda mrefu. Ni kwamba Shekha anapenda anacho kifanya ana jitahidi kusomea na kutembea sehemu mbalimbali kujua soko linataka nini.

Mwingine ambae tunaona ana jitahidi ni Flaviana Matata na product yake ya Lavy japo haina miaka mingi lakini imedumu katika soko na yeye kuanzisha service ya door to door kwamba anavijana wake wasafisha na wapakaji rangi kucha wana kuja mpaka ulipo kukupa huduma tuna hisi itafika mbali sana.

Lakini wapo ambao wapo kama hawapo na hata hawajulikani kama wapo. Je unajua Mwanamitindo wa kimataifa Tausi Likokola ana Hair Line yake iitwayo Tausi Beautiful Hair lakini pia alizindua perfume yake iitwayo Tausi Dreams, Hatujajua Tausi ana kwama wapi lakini hizi product zipo sokoni kwa muda sasa lakini ni wachache ambao wanajua kama ana brand ya aina hizi, hii inatokana na Tausi mwenyewe kuto kubrand sana brand yake lakini pia wa-Tanzania kutokuwa na muda wa kujua nini kinapatikana kwetu wengi wana kimbilia vitu vinavyo toka nje.

Jokate na Kidoti hair, well miaka miwili nyuma Kidoti alikuwa ana hype sana na brand yake mara kwa mara alikuwa ana post na kuwajulisha watu nini kipya kimeingia na kutumia muda wake mwingi kuji-brand inawezekana kidoti hair bado zipo sokoni lakini wengi wanaweza kuwa wamesahau hata kama Jokate ana hii brand kutona na yeye mwenyewe kuwa kimya. Tukiwaangalia wenzetu hapo Nchi za jirani kama Kenya kuna Hudda ambae ana lipstick zake na ukitembelea social networks zake ni mara kwa mara ana post kuhusu biashara yake kwanini wa kwetu wana jisahau? ni kuridhika au?

Chibu Perfume hizi zilikuwa perfume za Diamond Platnumz na kila mtu alikuwa ana zisubiri lakini guess what? zilikuja kwa mkupuo wakati mmoja tu na hatukusikia tena, labda soko halikuwa kubwa au hawakufikia lengo lakini haimaanishi waache kabisa kutengeneza bidhaa hizi bali ni kuangalia soko lina taka nini na kulipatia, kama ukimuangalia Diamond ni brand ambassador wa balaire kinywaji cha Rick Ross japo wengi wanasema si chake lakini ana jaribu kukipush World Wide na unaweza kuona Diamond anavyo ki-promote utashangaa wakati bidhaa yake yeye mwenyewe hatukumbuki mara ya mwisho lini kukipost.

Kiss By Wema ilipoteaga tu juu ya hewa na hakuna kipya mpaka sasa tumeambiwa tu save the date mpaka June hopeful its something big na sio longolongo tulizo zoea, Kiss by Wema Sepetu ilikuwa ifike mbali maana alisha pata mawakala mpaka nje ya Nchi na yeye kwake alikuwa ana promote sana what happened hatujui kama kala mtaji au ameamua kupumzika.

Wapo ambao wana jaribu kuja na bidhaa zao kwa mfano kwa sasa Hamissa Mobetto amekuja na lipstick tunaomba zikae sokoni na zikue, inawezekana soko ni dogo au baya lakini we need to push kuwa na hivi vitu vya kwetu wenyewe, its nice ukiwa una m-support mtanzania mwenzio sio kina Hudda Beauty na Mac kila siku wakati vya nyumbani vipo pia.

 

Related posts

4 Comments

 1. https://w.ytmp3.bz

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/kwanini-uwekezaji-katika-urembo-tanzania-unazorota/ […]

 2. 1 up mushroom, 1up mushroom

  … [Trackback]

  […] There you can find 20007 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/kwanini-uwekezaji-katika-urembo-tanzania-unazorota/ […]

 3. steroide online kaufen erfahrungen

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/kwanini-uwekezaji-katika-urembo-tanzania-unazorota/ […]

 4. รับแพ็คสินค้า

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/kwanini-uwekezaji-katika-urembo-tanzania-unazorota/ […]

Comments are closed.