Leilan ni Mtanzania ambaye alikuwa India kujifunza maswala mazima ya make up,Leilan ambaye kwasasa amerudi nchini Tanzania akiwa amefungua darasa la kufundisha maswala ya make up pamoja na urembo kwa ujumla.
Akiongea na Afroswagga ofisini kwake Tabata Segerea alisema “Nipo Tanzania natamani sana kufanya kazi na wasanii wa hapa lakini changamoto niliyonayo ni kwamba hawanifahamu.Na kama akitokea msanii au wasanii basi mimi nipo tayari maana sichagui mtu wa kufanya nae kazi. Lakini India niliwahi kushiriki kufanya make up washiriki wa filamu ya Chamand Karoh na Got talent hili ni tamasha kubwa pale india na make up nilifanya mimi. Pia kuna vitu vingi watu inapaswa watu wajue hasa tofauti ya make za event na video music,ambapo tofauti ipo katika event za kawaida inabidi utumie cream hasa, na video music utumie powder shauri ya camera zaidi lakini huwa naona watu wanajichanganya.
Naona hata mitaani wakina dada walio wengi wanapenda sana maswala ya kujua au kujifunza make up,lakini hawajui waende wapi.Mimi nipo wanaweza kuja muda wowote na kujifunza zaidi juu ya make up.”Alisema
Video chini akiwa anamfanyia mmoja ya wadada make up.
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/leilan-beuty-mtanzania-kwenye-filamu-ya-chamandi-karoh-india/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/leilan-beuty-mtanzania-kwenye-filamu-ya-chamandi-karoh-india/ […]