SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Lulu Diva Na Muwasho Wa Wig
Urembo

Lulu Diva Na Muwasho Wa Wig 

Mwanamuziki, mtangazaji na muigizaji Lulu Diva ameonekana katika kipindi cha Mr. Right hivi karibuni akiwa anajipiga piga kichwa hii ni ishara ya kwamba wig yake ilikuwa ina muwasha na alikuwa ana jaribu kupunguza muwasho huo.

Kwa msanii mkubwa kama yeye hii hali haileti picha nzuri kwa maana moja ya sababu ya wig au nywele kuwashwa ina husishwa na nywele kuwa chafu, well baada ya kuona hili tumeona tuwaletee sababu na namna ya kuzuia aibu hii isitokee tena

Sababu za kwanini nywele yako inawasha

 • Nywele zako za asili ni chafu

Mara nyingi tunaovaa wigs au kusukia weaving tunajisahau kwenye kusafisha nywele za asili kwa maana zinafichwa na hii husababisha uchafu kuzaliana ukakutana na joto basi lazima muwasho utokee.

 • Una Mba

Mba ni tatizo kubwa kwa wengi wetu kama una mba na ukavaa wig lazima utapata miwasho mara mbili na ukiwa hujavaa wig au kushonea weaving.

 • Una Allergy Na Shampoo / Vipodozi Vya Nywele Unavyotumia

Unapaswa pia kuzingatia ni bidhaa gani unatumia kwenye nywele zako na wigi yako kwani unaweza kuwa na mzio kwa baadhi ya viungo.3

 • Hujakausha Nywele Zako Za Asili Vyema

Kama nywele zako za asili hazijakauka vyema unaweza kupata hisia ya kuwasha, pia. Kwa hivyo hakikisha unakausha nywele zako asili vizuri kabla ya kuvaa wigi kwa sababu unyevu kupita kiasi unaweza kusababisha miwasho.

 • Ukosefu Wa Hewa Kati Ya Kichwa Chako Na Wig

Kama hakutokuwa na nafasi ya hewa kati ya wig na kichwa chako, kichwa chako hakiwezi kupumua hivyo kusababisha jasho na unyevu kupita kiasi na kuleta miwasho.

Nini Ufanye?

 • Safisha nywele zako kabla ya kuvaa wig
 • Tumia bidhaa za asili za nywele kusafishia nywele zako ili kuepuka allergy
 • Hakikisha nywele zako za asili zimekauka vyema kabla ya kuvaa wig
 • Tumia dawa za kutibu mba kabla ya kuvaa wig yako
 • Chagua cotton wig cap ili nywele ziweze kupitisha hewa, na kuepuka ukaukaji wa ngozi na miwasho
 • Nunua wig yenye quality nzuri


																			

Related posts