SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MAFUTA YA ALIZETI KWA UBORA WA NYWELE ZAKO
Hair

MAFUTA YA ALIZETI KWA UBORA WA NYWELE ZAKO 

Mafuta ya alizeti yanasifika kwa kuwa na fatty acids muhimu pia antioxidants muhimu zinazoweza kufaa katika kuzipa afya nywele zako pamoja na ngozi ya kichwa.
Mafuta ya alizeti yanasaidia watu wenye nywele kavu na ngozi ya kichwani inayowasha (itchy scalp), yatakusaidia kulaininsha nywele na kupunguza au kuondoa kabisa ile hali ya kichwa kuwasha.

Namna ya kufanya Treatment na mafuta ya alizeti pekee

Mahitaji
1. Mafuta ya alizeti
2. Chanuo au kitana kikubwa
3. Taulo lililowa maji ya moto/uvuguvugu

Jinsi ya kufanya

  • Osha nywele zako ziwe safi, chukua mafuta ya alizeti ya kutosha paka kwenye nywele zako yakolee. Unaweza kuchana na kitana kikubwa ili kuyafikisha kwenye ncha za nywele zako.
  •  Jifunge kichwani taulo lako lililowa maji ya uvuguvugu ili kuzipa nywele unyevu na joto mafuta yaweze kupenya vizuri katika nwele zako.

Pia unaweza kuyatumia mafuta ya alizeti kwa kuchanganya na mafuta yako mengine ukayatumia kama base kwa kuwa ya bei rahisi, kisha unatia yale ya gharama kidogokidogo  mfano unaweza kufanya mchanganyiko ufuatao:-

  • Mafuta ya alizeti
  • Castor Oil kidogo
  • Almond oil kidogo
  • Argan Oil kidogo au hata ya nazi

Mchanganyiko huu unaweza kuutumia kama treatment hapo juu au unaweza kuyapaka mara mbili kwa wiki kwa kuweka katika chupa yenye kipakio.

Yapo mafuta ya alizeti yaliyotengenezwa kwa ajili ya nywele lakini unaweza kukuta ni gharama na yameongezewa  kemikali nyingine nyingi, tumia yaliyo karibu.

Related posts

2 Comments

  1. buy boring cart

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/mafuta-ya-alizeti-kwa-ubora-wa-nywele-zako/ […]

  2. buy psilocybin mushrooms united states​

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/mafuta-ya-alizeti-kwa-ubora-wa-nywele-zako/ […]

Leave a Reply