Black Castor oil ni mafuta ya mnyonyo tofauti ya mafuta ya mnyonyo,tofauti ya mafuta haya na mengine ya mnyonyo ni kwamba Black Castor Oil yanatengenezwa kiasili bila kuondolewa au kuongezwa vitu katika uhalisia wake, wakati mafuta ya mnyonyo mengine hupitia viwandani kutengenezwa na kuongezwa vitu vingine vingi.

Kama ambavyo tunakua kitu kinachopia katika kiwanda mara nyingi hupunguzwa ubora wake kwa kemikali ambazo huongezewa katika kitu hiko, lakini vile ambavyo hutengenezwa kiasili na kuachwa na asili yake huwa na ubora waasili ambao unamatokeo mazuri zaidi.
Sifa Za Black Castor Oil
- Ina ricinoleic acid
Ambayo husaidia mzunguko wa damu kichwani, hii husaidia virutubisho kufika katika nywele zako na kusaidia ukuaji wa nywele
- ricinoleic acid
Asidi hii iliyopo katika black castor oil husawazisha pH ya ngozi yako na ina antibacterial, antifungal, na anti-anti-inflammatory. Hii husaidia kuondoa maambukizi ya ngozi, bakteria, na mba uliopo kwenye ngozi ya kichwa kuoneoka
- antioxidants
Hii husaidia keratin kwenye nywele zako. Hii hufanya nywele zako kuwa na nguvu, muundo zaidi, laini, na kutokakamaa. huimarisha Mizizi ya nywele pia inapunguza upotezaji wa nywele, na kuifanya JBCO kuwa tiba nzuri kwa alopecia.
- Omega-6 and Omega-9 fatty acids
Husaidia kuipa nywele yako unyevu
Mafuta haya ya mnyonyo yana faida mbalimbali lakini wengi tunajua faida za katika nywele ambapo hukuza nywele, ku repair damaged hair na hata kujaza nywele lakini je wajua unaweza kutumia kwenye ngozi pia? Yes unaweza kutumia mafuta haya kwenye ngozi nakukuletea matokeo mazuri kwa sababu yana vitamin E abayo ni nzuri kwenye ngozi.
faida za mafuta ya black castor oil katika ngozi
- Huondoa Chunusi
black castor oil ina mega 9 fatty ambayo ina saidia kuondoa chunusi unacho hitaji ni vitu vitatu pamba, black castor oil na mvuke wa maji ya moto.
Unacho takiwa kufanya ni:
- Chukua kiasi kidogo cha mafuta ya black castor oil paka katika uso wako katika sehemu zilizo athirika na chunusi
- acha mafuta hayo katika sehemu hio kwa dakika kumi kisha futa uso wako na kitambaa cha pamba ambacho ulikitumbukiza kwenye maji ya moto.
- Rudia hivi mara mbili kwa week kupata matokeo ya haraka
- Kasaidia kuondoa mikunjo ya uzee
Nani anataka kuzeeka mapema? Sote tunataka kuwa vijana well kama una mikunjo au hutaki kabisa kuona usoni mwako hata kabla hujaanza kuiona unaweza kutumia black castor oil,
- black cator oil kama una cleanser tumia cleanser kusafisha uso wako kama huna tumia ndimu,
- safisha uso kisha ufute uwe mkavu,
- paka black castor oil katika sehemu zilizo athirika kwenye mikunjo,
- wataalamu wanasema fanya hivi mara mbili kwa siku kupata matokeo mapema lakini pia ni vizuri ukifanya kabla ya kulala.
Black castor oil imekuwa review na watu takribani 4000 katika mtandao wa Amazon na kati ya hao 70% wameyapa hadhi ya 5 star. Pia tulipost Instagram na wengi wameonekana kuyapa matokeo chanya.
View this post on InstagramA post shared by AfroSwagga 🇹🇿 (@afroswagga) on
Tuambie umeshawahi kutumia mafuta haya? na je matokeo yake yalikuwaje?
Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda se… https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…