SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Majani Ya Mlonge Na Msaada Wake Katika Urembo
Urembo

Majani Ya Mlonge Na Msaada Wake Katika Urembo 

Majani haya yana kiasi kikubwa cha madini  sulphur na Vitamin E ambazo ni asilia Kabisa na ni muhimu Sana  katika urembo.Majani haya yana uwezo wa kupendezesha nywele zako pamoja na kuzifanya zikue vizuri zaidi, Pia yatapendezesha ngozi yako na kuiacha iking’aa pamoja kuondoa chunusi.

JINSI YA KUTUMIA MLONGE  KATIKA NGOZI

 Unaweza kutengeneza facial toner kwa kuchemsha majani  yako ya mronge kisha uyaweke kwenye fridge tayari kwa matumizi, Jitahidi ndani ya siku 3 hadi 5 Utengeze Mpya.

➡ Unaspray usoni ama utapaka kwa kutumia pamba safi na baada ya robo saa utaosha kwa maji ya kawaida.

Pia unaweza kutengeneza mask ya mronge kwa ngozi nyororo kabisa

 • Mahitaji
  ➡ unga wa majani ya mronge
  ➡ Unga wa mdalasini
  ➡Maziwa
  ➡Asali
 • Jinsi ya kufanya
  ✔ Changanya mahitaji yote pamoja kisha changanya vizuri.
  ✔Paka usoni na baada ya robo saa unaweza kunawa kwa maji ya kawaida.

JINSI YA KUYATUMIA KATIKA  NYWELE ZAKO

Unaweza kutengeneza hair tonic kwa kutumia majani haya

✔ Chemsha majani yako Kisha yachuje na maji yake utaoshea nywele zako….

✔ Pia unaweza kuyatumia kama prepoo Yaani Kabla ya kuosha kwa shampoo,  utasaga kwenye blender kisha ukamue juice yake na upake kwenye ngozi ya kichwa chako baada ya saa moja  utaosha..

 Unaweza pia kutengeneza mafuta kwa majani haya kwaajili ya ukuaji mzuri wa nywele zako.

 • Mahitaji
  ➡Mafuta ya nazi pure/zeitun
  ➡Unga wa majani ya mronge….
 • Jinsi ya kufanya
  ✔ Weka unga wa mronge kwenye bakuli safi kisha mimina mafuta yako na uyafunike.
  ✔ Baada ya siku 3 funua mafuta yako chuja vizuri ukiyafunua bila ya shaka.yatajitenga mafuta na makapi….
  ✔ Usichanganye na makapi chuja mafuta tu na yatakua tayari kwa matumizi.
  ✔Tumia mafuta haya kila siku ukihakikisha unayafikisha kwenye ngozi ya kichwa chako na ukimassage isipungue dakika 5 kila siku….

Je ulikuwa unafahamu namna ya kutumia mronge!? Tuambie kwenye comment hapo chini!

Imeandaliwa na Kuandikwa Na @bint_Urembo

Related posts