Tunapenda kupaka make ups na urembo mwingi lakini wakati mwingine hazitokei sahihi na matarajio yetu.
Kwa sehemu kubwa picha zinazosambazwa mitaani kupitia mitandao ya kijamii ni za dada zetu,rafiki zetu na hata mama zetu ambao hawajui kitu ila tu wanaamini wakipaka tu Angel face/Powder au Foundation uliyopaka wewe watakuwa vizuri. Ni wakati tuhurumiane na kushauriana si kumpiga picha ndugu yako akiwa ameshaharibikiwa sura.
Kinachofanya Make Up yako iwe On Point
1. Rangi sahihi inayoendana na ngozi yako
Unapochagua Foundation na poda ni vema ujue na uchague rangi sahihi sio kufuata kauli ya muuza vipodozi kwamba hii ya mweupe au hii ya mweusi. Watengenezaji wa hizi bidhaa wameziweka kwa “range” ya rangi ili kila tu apate inayoendana au kukaribiana.
Sijui lengo ni blushes? watu weusi hatuna asili ya kublush hivyo hizi rangi tunahitaji umakini zaidi maana unaweza kuhurumiwa kwamba umepigwa
.Tumia kifaa sahihi
Iwapo ni kublend tumia sponge ya kublend, iwapo ni kupaka tu poda tumia kipakio au brashi laini ili vipodozi vikae mahali pake na kwa kiwango chake.
Sponge za kublend make up, hasa ukitumia concealer ili uiblend vizuri
Brushes mbali mbali kwa matumizi tofauti tofauti
3. Usipoteze uhalisia
Iwapo unajua nyusi za mtu mweusi ni nyeusi kwa nini uweke nyekundu? na position ya nyusi inaendana na mkao wa fuvu lako, kwa nini uziache mbali nyusi na mchoro ukapanda juu sana? Jaribu kuzingatia uhalisia katika kujiremba.
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/make-up-sahihi-ni-pamoja-na-vifaa-sahihi/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/make-up-sahihi-ni-pamoja-na-vifaa-sahihi/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/make-up-sahihi-ni-pamoja-na-vifaa-sahihi/ […]