Wote tunaosha nywele ila haitakushangaza ukisikia kwamba uoshaji wa nywele zako si sahihi. Wengi wetu tumekuwa tukifanya makosa kadhaa wakati wa kuosha nywele. Baadhi yetu hatutumii muda wa kutosha kusugua scrub” ngozi ya kichwa “scalp”, hatuoshi vizuri na baadhi pia hatutumii conditioner. Na haya ni baadhi tu ya mambo ambayo tunakosea wakati wa kuosha nywele.
Leo utajifunza namna sahihi ya kuosha nywele ili uziache nywele zako zikiwa safi kana kwamba umeziosha kwa mtaalamu wa saluni.
Yafuatayo ni makosa makubwa matano watu wengi huyafanya wakiwa wanaosha nywele…
- Kutolowanisha nywele vizuri.
Watu wengi hawaloweshi nywele zao vizuri kabla ya kupaka shampoo. Ni muhimu kulowesha kila unywele kwa maji kabla ya kupaka shampoo. Kila nywele inahitaji kuloweshwa, kisha ipakwe shampoo ili ipate kutakata vizuri.
- Kutumia shampoo nyingi sana au kidogo sana.
Wote tunafahamu kwamba kitu chochote kikizidi kina madhara au hakitaleta matokeo mazuri. Tunatakiwa kutumia kila kitu kwa kiasi. Si kwa wingi sana na si kwa uchache sana. Kanuni hii pia inatumika kwenye upimaji wa kiasi cha shampoo cha kutumia wakati wa kuosha nywele.
Kutumia shampoo nyingi kunaweza kukufanya usiweze kuipata nywele na kuisafisha vizuri kutokana na kuzidiwa na povu jingi sana. Na kutumia shampoo kidogo kutafanya nywele zako zisitakate vizuri. Pima shampoo kiganjani kwako, kiasi cha wastani kulingana na ukubwa na wingi wa nywele zako, kwa kutumia vidole paka shampoo kwenye nywele zako ulizozigawanya kwenye makundi manne. Paka kuanzia kwenye ngozi ya kichwa “scalp” kuja kwenye ncha ya nywele.
- Kutotilia maanani zaidi ngozi ya kichwa.
Kama umeshawahi kufanyiwa shampoo kitaalam saluni bila shaka unajua ni muda kiasi gani huwa wanautumia kwenye ngozi ya kichwa. Kusugua ngozi ya kichwa ni hatua ya msingi zaidi kwenye mchakato wa kuosha nywele.
Watu wengi hawatumii muda wa kutosha kusugua ngozi zao za kichwa. Tunatakiwa kusugua ngozi zetu za kichwa kwa walau dakika tatu. Bila kujali urefu au aina ya nywele zako unachotakiwa ni kusugua ngozi yako ya kichwa. Na unatakiwa kufanya hivyo kwa kutumia vidole na sio kucha kwa muda usiopungua dakika tatu.
- Kutokuosha na kurudia “rinse &repeat”
Ni muhimu sana kuosha nywele na kurudia. Na hii ni muhimu zaidi kwa wale wenye nywele ndefu. Kama una nywele fupi au ndogo kabisa si lazima kwako kuosha na kurudia. Baada ya kuwa umesugua ngozi ya kichwa “scalp” kwa dakika tatu, ni muda wa kuosha nywele. Ukishaosha inafuata hatua ya pili ya uoshaji wa nywele. Unatumia shampoo kama kawaida. Kwenye hatua hii utaweka msisitizo zaidi kwenye nywele zenyewe kwakuwa tayari ngozi ya kichwa ulishashughulika nayo kabla. Mara hii weka msisitizo zaidi kwenye kuosha nywele zako na hakikisha hakuna nywele inayoachwa bila kupata shampoo kuanzia kwenye mzizi mpaka kwenye ncha.
- Kutokutoa shampoo vizuri kwenye nywele.
Baada ya kurudia kuosha nywele kwa mara ya pili kinachofuata ni kutoa shampoo kwenye nywele.
Watu wengi hawatoi shampoo vizuri kwenye nywele, na hii huzifanya nywele kubaki na shampoo ambazo zinasababisha nywele kubaki na vitu vyeupe vyeupe “build-ups” na nywele pia kutosafishika vizuri. Hivyo inasisitizwa kutumia muda na maji ya kutosha kutoa shampoo na kuhakikisha imetoka kabisa kwenye nywele ili nywele zako ziwe zimesafishika vizuri.
Yapo makosa mengi sana ya utunzaji wa nywele yakianziwa na uoshaji wa nywele. Ila tukianza kuyasahihisha baadhi ya makosa tuliyoyaelezea hapo juu na kuanza kufuata utaratibu mzuri wa uoshaji wa nywele naamini sote tutakuwa tumeanza safari nzuri ya kuelekea kuwa na nywele nzuri na zenye afya!
Related posts
HOT TOPICS
We need to have some sort of bima ila for enjoyment. Yaani wanakata ka % ka mshahara kako unakua na card ukienda se… https://t.co/W9oDoaN2YY
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…