SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mambo 3 ya muhimu kuyajua unapotaka kuwa na dreadlocks
Urembo

Mambo 3 ya muhimu kuyajua unapotaka kuwa na dreadlocks 

Nimekuwa na dreadlocks kwa miaka miwili sasa, na mimi ni mmoja wa wale tulioanza kunyoa kwanza halafu kuanza ukursa mpya kabisa na mtindo huu wa nywele. Ukweli ni kuwa dreadlocks ni mtindo wa nywele ambao hauna kazi kubwa sana ukilinganisha na mitindo mingine, lakini ni muhimu sana kuziangalia na kuzijali maana unaweza kuziharibu kwa kutokuzijali. Kama unataka kuwa na dreadlocks, hay ani mambo 3 ambayo nilitakiwa kuyajua toka naanza, sema nakushirikisha ili usichelewe kuyajua kama mimi nilivyochelewa;

  1. Nywele huwa zina asili tofauti, usijitese kwa kulinganisha ukuaji na ubora wa nywele

Kuna wale ambao wananywele nyingi, wengine nyepesi, wengine zinakua haraka, wengine zina rangi Fulani nk. Hata kama umeanza kutengeneza dreadlocks na rafiki yako, ukuaji huwa tofauti, ruhusu nywele zako kukua vile zinavyotaka na usijipe shida ya kulinganisha au kutamani zikue katika namna Fulani. Maisha mafupi, acha nywele zako ziku-surprise na ridhika na ukuaji wake.

  • Kwenye jamii zetu kuna mitindo bado inaangaliwa kwa jicho la tofauti, dreadlocks zikiwemo

Unajua ukiwa na dreadlocks ukikatiza tu sehemu Fulani wanaweza kudhani wewe ni mtu wa namna Fulani. Nilichojifunza ni kuwa dreadlocks zilinifanya kujikubali vile nilivyo na kutojali watu wananidhaniaje, kutoruhusu mawazo yao kunisumbua kwasababu mwisho wa siku Maisha yangu ni mimi ndio naamua jinsi ya kuyaishi, nywele zangu mimi ndio naamua mtindo wa kuwa nao. Kama unataka kuanza, usiruhusu watu wanavyokufikiria ikusumbue kiasi cha kwamba hauanzi kwasababu yao, kama unapenda na una uwezo wa kufanya, fanya.

  • Dreadlocks zina vipindi tofauti katika ukuaji, jipende na uzipende wakati wote

Kuna kipindi kinaitwa ‘ugly stage’, hiki ni kile ambacho nywele ni ndogo sana na hata haziko muonekano ambao utapenda watu wakuone nazo. Lakini bado katika hali hiyo jiangalie kwenye kioo na ujikubali, ujipende katika hali zote. Kujipenda na kujikubali ambako nimekupata kutokana na kuanza safari yangu ya dreadlocks kumenisaidia sana hata kujiamini. Kuwa mvumilivu wakati zinakuwa, jifunze kupenda na kujipenda katika kila hatua ya ukuaji.

Mwisho wa siku ni muhimu kujua kuwa nywele zinaongezea utofauti na kujiamini kwako, usiogope kuwa dreadlocks maana ni mtindo ambao kwa nywele za Kiafrika unapendezea sana.

Imeandikwa na Eunice Tossy, Freelance Writer (https://www.clippings.me/eunicetossy)

Related posts

5 Comments

  1. Where to buy DMT Brisbane

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-3-ya-muhimu-kuyajua-unapotaka-kuwa-na-dreadlocks/ […]

  2. DMT Vape Pens For Sale Brisbane

    … [Trackback]

    […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-3-ya-muhimu-kuyajua-unapotaka-kuwa-na-dreadlocks/ […]

  3. Golden Teacher grow kit

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-3-ya-muhimu-kuyajua-unapotaka-kuwa-na-dreadlocks/ […]

  4. 다시보기

    … [Trackback]

    […] There you will find 30520 additional Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-3-ya-muhimu-kuyajua-unapotaka-kuwa-na-dreadlocks/ […]

  5. Cold fir cartridges https://exotichousedispensary.com/product-tag/cold-fire-cartridge/

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-3-ya-muhimu-kuyajua-unapotaka-kuwa-na-dreadlocks/ […]

Comments are closed.