SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mambo Manne (4) Kuhusu Urembo Unapaswa Kujua
Urembo

Mambo Manne (4) Kuhusu Urembo Unapaswa Kujua 

Sote tunapenda kuwa warembo, beautiful skin, nice hair (long or short), nails nakadhalika na hii hutupelekea kuwa tuntafuta bidhaa ambazo zitatufanya tuonekano warembo lakini kuna baadhi ya mamabo ambayo huwa tunasahau kwamba yapo na yanaweza kutuletea madhara, leo our girl @style.with.mimi anakukumbusha baadhi ya vitu abavyo unapaswa kuvijua katika utumiaji wa bidhaa za urembo

Bidhaa za urembo hu expire

Hili ni jambo ambalo inawezekana unalijua lakini hailifuatilii sana.Wengi tukinunua vipodozi tunapaka mpaka siku kitakapoisha bila kujali kama huo ni muda sahihi wa kukaa na kipodozi au lah! Kwa baadhi ya vipodozi kuna alama kama iliyozungushiwa kwenye picha.

Hiyo alama inaonyesha idadi ya miezi ambayo unapaswa kutumia kipodozi mara baada tu ya kukifungua. Kwa bidhaa ambazo hazina maelekezo huu ndio muda sahihi wa kukaa na vipodozi mbalimbali;

  • Sponge aina zote ( mwezi 1-2)
  • Lotion aina zote (mwaka 1)
  • Shampoo na bidhaa za kustyle nywele (miaka 2)
  • Cream za kunyolea (miaka 2)
  • Deodorant,sabuni,mouthwash (miaka 3)
  • Mascara na wanja wa maji (miezi 3)
  • Foundation na concealer za maji (Mwaka 1)
  • Make up kavu za powder,Lipstick,lipgloss,wanja mkavu (Miaka 3)  

Kuna bidhaa za ngozi zinazobadili umbo na muonekano

Kila unachopaka kwenye ngozi yako huathiri mwili wako kwa namna moja au nyingine kama ilivyo kwa vitu unavyokula na kunywa. Vitu unavyopaka hupenya ndani ya mwili wako na mabaki,uchafu,sumu huchujwa kwenye ini.Baadhi ya bidhaa za urembo hubadili mfumo wa mwili hata kusababisha mtu aongezee uzito, atunze mafuta kiunoni na tumboni zaidi na hata kuotesha ndevu kwa mwanamke.Vipodozi vyenye corticosteroids (moja ya ingredients katika dawa za ngozi) ni moja ya vitu vinavyoweza kuleta madhara hayo.Corticosteroid huwekwa kwenye dawa za ngozi na hushauriwa kutumika si zaidi ya wiki mbili lakini uwezo wa baadhi ya  corticosteroid kubadili rangi ya ngozi umefanya dawa hizi zitumike kwa muda mrefu sana tena kama lotion za kila siku na baadhi ya watengenezaji wa bidhaa za urembo pia huziweka katika bidhaa zao kinyume na sheria. Corticosteroid zipo aina nyingi na baadhi ni clobetastole na betamethasome. Mfano wa lotion zenye Corticosteroid ni lotion maarufu ya CLONOVATE. Pia ingredients kama trichosan na phthalates huharibu balance ya hormone hivyo kuchangia katika kufanya mwili unenepe hovyo.Unaponunua bidhaa ni kuhimu kuchunguza vitu vilivyomo.

Natural/asili haimaanishi sahihi na isiyo na madhara.

Kumekuwa na muamko wa matumizi ya bidhaa asili sana. Kiujumla vitu asili ni bora zaidi kuliko vitu vinavyotengenezwa kiwandani na kuwekewa kemikali nyingi. Pamoja na hilo kumbuka si kila kilichoandikwa asili basi ni asili kweli hivyo nunua kutoka kwa mtu anayeaminika. Pia kuna vitu ambavyo vina bidhaa asili au ni asili lakini vinaweza visiendane na ngozi yako au mwili wako kiujumla. Baadhi husababisha hata madhara ya allergy.

Hakikisha unaijaribu product kwenye sehemu ndogo ya ngozi yako. Pia kuna michanganyiko ya vitu asili ambayo si salama kwa ngozi yako na mwili mfano mitishamba inayopunguxa mwili kwa kuharisha, scrub za sukari au chumvi yenye vipande vikubwa kwa ngozi ya usoni (husababisha vichubuko midogo/micro tear). Baadhi ya vitu asili hupulizwa madawa mengi vikiwa shambani na baadhi ya haya madawa si mazuri kwa ngozi. Unaweza kutumia bidhaa asili na bado utokwe vipele vingi. Fanya mazoea ya kuchunguza vitu unavyotumia hata kama ni asili.

Kupumzisha mwili (Too much of anything is harmful)

Ukizidisha kitu chochote kuna uwezekano mkubwa wa kupata madhara. Ukikaa na make up muda mrefu, ukifanya scrub mara nyingi sana au kwa nguvu sana. Ukinywa maji mengi kupitiliza, ukisafisha uso mara nyingi,ukifanya mazoezi mengi sana, ukikaa kwenye jua muda mrefu. Kuwa na kiasi katika shughuli zako za urembo na afya,pumzika na pumzisha mwili. Wingi si ubora.

Related posts

5 Comments

  1. Plantation Shutters

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-manne-4-kuhusu-urembo-unapaswa-kujua/ […]

  2. Psilocybe Cubensis B+

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-manne-4-kuhusu-urembo-unapaswa-kujua/ […]

  3. weed delivery toronto

    … [Trackback]

    […] There you can find 88057 more Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-manne-4-kuhusu-urembo-unapaswa-kujua/ […]

  4. window installer

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-manne-4-kuhusu-urembo-unapaswa-kujua/ […]

  5. Dividend

    … [Trackback]

    […] There you will find 7294 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-manne-4-kuhusu-urembo-unapaswa-kujua/ […]

Comments are closed.