SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mambo Matano Usiyoyajua Kuhusu Mafuta Ya Nazi
Urembo

Mambo Matano Usiyoyajua Kuhusu Mafuta Ya Nazi 

Mafuta ya nazi ni mazuri kama yatatumika ipasavyo.yana uwezo wa kukufanya uonekane mrembo mwenye ngozi ya kuvutia.

Miongoni mwa faida tano za kutumia mafuta ya nazi asilia ni kama ifuatavyo. 

  • Kulainisha ngozi

Kuondoa magaga kwenye nyayo za miguu kuzuia mipasuko ya nyayo za miguu kukauka kwa ngozi ya mikononihivyo mafuta yanazi yanasaidia kwa kiasi kikubwa sana kulainisha ngozi na kuipa afya nzuri.

  • Kuondoa ngozi iliyoharibika” Dead skin”


Mafuta ya nazi husaidia kuondoa ngozi iliyoharibika katika mwili wako, chukua mafuta ya nazi, sukari na chumvi changanya upate mchanganyiko mmojakisha paka mwili mzima.


Fanya massage kwa mchanganyiko huo kaa nayo kwa mda kisha kaoge vizuri na sabuni.utaona tu mabadiliko katika ngozi yako baada ya zoezi hili.Fanya mara 3 kwa wiki au utakavyoamua wewe.

  • Kuondoa Make Up


Mafuta ya nazi yanaweza pia kutumika kuondoa makeup usoni baada ya kutoka kwenye sherehe ukiwa na makeup unashauriwa kuitoa kabla ya kuingia kulala ili kuendelea na ngozi nzuri yenye afya. Mafuta ya nazi yanatumika hivichukua pamba safi chovya kwenye mafuta ya nazi.
kisha anza kufuta uso wako taratibu kwa kutumia pamba iliyo na mafuta ya nazi. baada ya kufuta chukua cleanser uliyoandaa au nawa uso wako vizuri na sabuni.ukifanya haya utasaidia kutunza uso wako na kuwa na afya nzuri.

  • Kukuza nywele


Mafuta ya nazi, yanatumika katika kurutubisha nywele na kufanya ziwe na nuru na kujaza,kupaka kwenye ngozi kupaka sehemu ya nywele ambazo hafifu au zilizo katika.

  • Kusaidia katika kunyoa “Shave oil”


Wengi wetu tumezoea kutumia Shave cream wakati wa kunyoa nywele katika maeneo maeneo lakini mafuta ya nazi pia yanaweza tumika hapa badala ya shave cream, yenyewe yanasaidia kutibu vipele vinavyojitokeza baada ya kunyoa.


haya mafuta wengi wanatumia katika kunyoa vinyweleo, inakuacha ukiwa soft na inasaidia kwa kiasi kikubwa kukufanya ngozi yako iwe salama tofauti na kutumia kiwembe au kitu kingine.


Shea na uwapendao 
©binturembo 

Related posts