Kuchagua kipodozi sahihi ni jambo la muhimu katika swala zima la kutunza afya ya ngozi zetu. Kitu chochote tunachopaka kwenye ngozi ni muhimu zaidi ya vile tunavyo fikiri. Baadhi ya watu huchagua kipodozi kwa nia ya kutatua matatizo fulani ya ngozi zao, huku wengine huchagua ili kuwa na utaratibu unaofaa wa kutunza ngozi zao ziendelee kuwa na mvuto zaidi.
Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la vipodozi vinavyo semekana kuwa na uwezo wa kufanya ngozi ya mwili kuwa nzuri na ya kuvutia zaidi; hata wakati mwingine kusababisha vipodozi hivyo kuuzwa bei ghali. Lakini wazungu wanakwambia ‘The most expensive products aren’t necessarily the best’. Swali la kujiuliza, kwa uwepo wa vipodozi vingi sana sokoni, unawezaje kufahamu kipodozi kitakachofaa kwenye ngozi yako?
yafuatayo ni mambo 3 ya msingi ya kuzingatia wakati wa kuchagua kipodozi kinachofa kwa ajili ya ngozi yako.
- Aina ya ngozi (skin type).
Kabla ya kutumia kipodozi unapaswa kwanza kujua aina ya ngozi yako kama ni kavu(dry), ya mafuta (oily), mchanganyiko (combination) au ya kawaida (normal).Unaweza kutambua aina ya ngozi yako kwa njia rahisi; osha uso wako na usubiri kwa masaa machache bila kuupaka chochote kisha uutazame ukiwa katika muonekano wake halisi. Hapo utaweza kugundua aina ya ngozi yako. Katika makala zijazo nitakuja kuzungumzia kwa undani zaidi kuhusiana na aina za ngozi na njia za kuzitunza.
Jinsi Ya Kujua Aina Ya Ngozi Yako
- Ingredients
Kila kipodozi huwa na ingredients kadhaa katika mchanganyiko wake. Angalia kila ingredients na ujue kina kazi gani kwenye ngozi. Kutegemeana na aina ya ngozi yako unatakiwa kutambua ingredients za kuziepuka na zile zinazokufaa.
Ngozi kavu: Tafuta kipodozi kilicho changanywa na olive oil, jojoba oil, shea butter, lactic acid, glycerin, mineral oil au hyaluronic acid.
Ngozi ya mafuta: Tafuta kipodozi kisicho na mafuta yaani ‘oil-free’ ili kuzuia matundu ya ngozi yasijizibe kuepuka kupata chunusi.
Ngozi mchanganyiko: Tafuta kipodozi chenye alphahydroxy acid na betahydroxy. Epuka kipodozi chenye chemical fragrance na alcohol menthol.
- Expiration date.
Ni muhimu kuangalia tarehe ya kumalizika muda wa matumizi ya kipodozi. Kipodozi kilichokwisha muda wake kinaweza kubeba bacteria wanaoweza kusababisha muwasho, maambukizi katika ngozi hata kuleta muonekano wa ngozi usiofaa.
Kuna baadhi ya vipodozi hutumia period-after-opening symbol kama picha inavyoonekana hapo chini. Alama hii huonesha idadi ya miezi ambayo kipodozi kinapaswa kutumika mara baada tu ya kufunguliwa.
Cha kuzingatia; kipodozi kilicho faa kwenye ngozi ya mtu mwingine, si lazima kikufae wewe pia.
Baada ya kufahamu haya, sio vibaya na wewe ukatuambia vitu gani unazingatia kabla ya kununua kipodozi chako kwa kucomment hapo chini.
Writter/content creator:- Gift Reinhard Lisapita
Instagram:- @gift_reinhard
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-matatu-3-ya-kuzingatia-ili-kupata-kipodozi-kinachoifaa-ngozi-yako/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/mambo-matatu-3-ya-kuzingatia-ili-kupata-kipodozi-kinachoifaa-ngozi-yako/ […]
healing music
healing music
jazz piano music
jazz piano music