SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Manjano Na Faida Zake Katika Urembo
Urembo

Manjano Na Faida Zake Katika Urembo 

Manjano ni kiungo kinacho tokana na mti uitwao curcuma longa, mti huu una patikana sana kusini mwa bara la Asia. Kiungo hiki kina tumiwa kwa namna nyingi una weza kutumia kama kiungio katika chakula lakini pia hutumika kama urembo na kina saidia sana.

manjano ina tumika kama bidhaa ya uzuri kwa muda sasa,ni njia rahisi na pia ina faida kubwa katika ngozi. Kabla ya kuwa na bidhaa za madukani bibi zetu walikua wakitumia manjano kutibia matatizo ya ngozi zao

Faida za manjano katika ngozi:

1) hutibu chunusi–  manjano ina ufanisi mkubwa katika antiseptic ns  antibacterial ambazo husaidia kupambana dhini ya chunusi na vidonda usoni na kuupa uso wako muonekano mzuri na mbichi manjano husaidia pia kupunguza mafuta usoni kwa wale wenye nyuso zenye mafuta.

Mahitaji

 • Liwa- kijiko kimoja
 • manjano- kijiko kimoja
 • maji ya limao kiasi

changanya viungo hivi pamoja na kisha upake usoni na ukae navyo kwa muda usio pungua dakika kumi (10), kwa kuondoa chunusi changanya manjano na maji masafi na upake usoni ukae nayo kwa muda usio pungua dakika kumi na tano (15)

shutterstock_201136739_1443681123

2) barakoa (mask) kwa wenye ngozi zenye mafuta – manjano  yana manufaa katika ngozi zenye mafuta husaidia kupunguza mafuta na hio upelekea kupungua kwa chunusi usoni

Mahitaji

 • maji ya machungwa
 • liwa
 • manjano

changanya changanyiko huo na upake usoni kisha ukae nao kwa muda wa dakika 10-15 kisha uoshe kwa maji ya vuguvugu.

3) barakoa (mask) kwa ngozi kavu- Kama una ngozi kavu , unaweza kufanya mask ya  uso kwa kuchanganya 1 ute wa yai , 2 matone ya mafuta ya olive , maji ya limao na kuchanganya na manjano . Hii inaweza kutumika kwa maeneo yote kavu kama vile uso, shingo, elbows na magoti. ruhusu ikauke na  kisha safisha na maji ya  moto.

4) huondoa makunyanzi- Manjano ikichanganywa  pamoja na viungo vingine,ina  ufanisi katika kupunguza makunyanzi usoni . Unaweza kuandaa kwa kuchanganya unga wa manano pamoja na unga mchele na maziwa na juisi ya nyanya na kupaka juu ya uso wako na shingo kwa dakika 30 . Suuza  na maji vuguvugu. Hii itapunguza makunyanzi katika ngozi na  vile vile kuang’aza ngozi yako.

5) kuondoa stretch marks – manjano husaidia kung’aza au kufuta stretch marks changanya manjano na maziwa mgando/maziwa fresh/maji na kisha upake kwenye eneo lililo athirika.

Faida za manjano katika nywele

ukiachana na ngozi tu manjano pia husaidia katika ukuaji wa nywele pia hutibu baadhi ya matatizo kichwani

1) huondoa m’ba – changanya manjano na olive oil na paka kabla ya kwenda kuoga, kaa nayo kwa dakika 15 ndio uoshe

2) kupunguza kukatika kwa nywele – kukatika kwa nywele hutokana na kuumwa, kuto kula vizuri au msongo wa mawazo, kwa kuwezesha hili changanya asali na manjano na kisha uondoe kwa maji masafi.

Related posts

2 Comments

 1. buy sig spear

  … [Trackback]

  […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/manjano-na-faida-zake-katika-urembo/ […]

 2. 티비위키

  … [Trackback]

  […] There you can find 19628 more Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/manjano-na-faida-zake-katika-urembo/ […]

Leave a Reply