SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Facial Mask Ya Manjano, Asali, Ndimu Na Mtindi
Urembo

Facial Mask Ya Manjano, Asali, Ndimu Na Mtindi 

Shekha Manjano ni mmiliki wa kampuni ya vipodozi vya manjano na juzi aliweka beauty tip ya namna ambavyo una weza kutumia manjano,mtindi,ndimu na asali kuondoa chunusi.. na hivi ndivyo alivyo andika katika kutoa somo hilo

“Weekend yangu naimalizia kujipamper na homemade face mask. Kama unasaumbuliwa na chunusi, au unauso wenye mafuta mengi kama wangu basi mara moja kwa wiki tengeneza ‘Face Mask’ yako mwenyewe nyumbani ili kupata ngozi soft.

Vifaa vinavyohitajika ni kama ifuatavyo;

Mimi hupendelea Zanzibar Turmeric Powder. Hii ni binzari ya Manjano hupatikana masokoni na supermarmets. –

Vijiko viwili (2 tbs) vya unga wa binzari ya Manjano (Turmeric powder)

– Kijiko kimoja (1 tbs) cha unga wa Riwa – wengine huita Liwa (Sandalwood powder)

– Vijiko vitatu (3 tbs) Mtindi (yoghurt)

– Nusu kijiko (1/2 tbs) maji ya ndimu (lemon juice)

– Kijiko kimoja (1 tbs) Asali ya bibi (honey)

Kwanza safisha uso wako kwa sabuni uwe msafi.

Changanya vyote kisha upake usoni (kasoro eneo lililozunguka jicho). Kaa nayo usoni mpaka ikauke au kwa muda wa dakika 10 – 15.

Kisha nawa uso wako kwa maji ya vuguvugu – usitumie sabuni.

Kama unazo chunusi nyingi, fanya hivi mara 3 kwa wiki na utaona mafanikio ya chunusi kuisha kabisa. Vilevile kama chunusi ulizonazo ni za muda mrefu, unaweza chukua glasi moja ya maziwa ‘fresh’; weka kijiko kimoja (tea spoon) cha unga wa binzari ya Manjano, vijiko viwili vya asali ya bibi, koroga na unywe – kunywa mara 3 kwa wiki (sio kila siku) – Itasaidia kuboost ‘immunity’ yako na pia kuisaidia system yako mwilini katika kutibu chunusi.

Kama huna chunusi kabisa fanya kujitengenezea face mask mara moja kwa wiki maana hii ni kinga hasa kama una uso wa mafuta (oily skin).

Related posts

3 Comments

 1. Buy DMT Vape Pen Australia

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/manjanoasalindimu-na-mtindi-facial-mask/ […]

 2. go to the website

  … [Trackback]

  […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/manjanoasalindimu-na-mtindi-facial-mask/ […]

 3. ozempic comprar sin receta, comprar ozempic online, ozempic comprar, comprar ozempic

  … [Trackback]

  […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/manjanoasalindimu-na-mtindi-facial-mask/ […]

Leave a Reply