SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Maoni Ya Madee Ally Na Nikki Wa Pili Kuhusu Makeup Na Urembo Bandia
Urembo

Maoni Ya Madee Ally Na Nikki Wa Pili Kuhusu Makeup Na Urembo Bandia 

Soko la urembo linazidi kukua Duniani, tunaona makampuni mapya ya vipodozi yakizinduliwa siku mpaka siku, watu maarufu pia wanaonekana kuvutiwa na soko hili.

Kama ilivyo kawaida kila jambao linapande mbili kuna wale watakao vutiwa nalo na wale ambao hawatotaka liendelee hata kidogo.

Week chache zilizopita wasanii wawili maarufu wa hiphop Madee Ally na Nikki wa Pili walitoa maoni yao kuhusu urembo wa makeup ambao wote wawili wakiwa na mitazamo hasi kuhusu urembo huo.

Ambapo alieanza ni Nikki wa pili ambae alisema yeye kwa upande wake anaona ma’bibi harusi wengi wakipaka makeup hawapendezi

Sisi hatujajua Nikki amewaona ma’bibi harusi gani au wa wapi, kwa sababu asilimia kubwa ya ma’bibi harusi huwa wanarembwa na wakarembeka hasa unless otherwise Nikki aliongea haya akiwa ameona wale mabibi harusi ambao hupakwa powder za baby Johson. Kama ukipata makeup artist ambae ni mzuri definitely utapakwa makeup na ukapendeza vyema kabisa.

Wakati Madee Ally yeye ugomvi wake ulikuwa na wanawake ambao wakiingia ndani ya ndoa wanaanza kujipodoa , akisema wanaume wengi wanasaliti (cheat) kwa sababu tu wakati anakuona hukuwa na kucha bandia, nywele bandia lakini baada ya kuwa nae umeanza kuweka hivyo vitu.

Neno letu ni moja tu kwa bwana Madee, mwanaume au mwanamke akitaka kukusaliti atakusaliti uwe natural kama uoto wa asili au ujibandike as long as anataka kucheat basi ata-cheat. Ni kama umwambie mwanaume wanawake wanacheat sababu wakati unakuwa nae ulikuwa na nywele na six pack lakini baada ya kuwa nae umekuwa na upara na kitambi.

Related posts