SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mapenzi Yake Na Kope Fake Yamemfanya Irene Uwoya Aje Na Bidhaa Ya Kope Fake
Make Up

Mapenzi Yake Na Kope Fake Yamemfanya Irene Uwoya Aje Na Bidhaa Ya Kope Fake 

Tukiongelea watu maarufu ambao tunajua toka zamani wanapenda kope fake basi ni Irene Uwoya, toka ameingia katika sanaa amekuwa akijulikana kutokana na mapenzi yake ya urembo huo, zamani alikuwa anapenda zile kope ndefu sana, kutokana na macho yake kuwa makubwa Irene always look great on long lashes.

Wakati siku zikiwa zinaenda na mambo yanamabilika, zikaletwa lashes bora zaidi na Irene hakuacha kuendelea kutumia, kama ambavyo watu maarufu wengi hupenda kutumia kile walicho nacho au walicho kikosa na kugeuza biashara basi ndivyo Irene Uwoya nae alipoona fursa ya mapenzi yake na kope bandia kuanzisha bidhaa yake ya kope hizo ambazo amezipa jina la I Lashes by Irene Uwoya kwetu sisi tunadhani hii ni move nzuri maana tumekuwa tukiona mapenzi yake na kope bandia, kitu ambacho tunataka kujua tu ni kwamba quality ni nzuri kama ambavyo packaging ilivyo.

Katika kurasa yake ya Instagram Irene aliandika kwanini ameamua kuja na bidhaa hizi

Habari,Ukiniita Oprah hutakuwa umekosea ila kwa majina niliyopewa na wazazi wangu ni Irene Pankras Uwoya.Ni kwa muda mrefu nimeweza kufanya vingi na kufanikiwa katika sanaa yangu ya uigizaji na yote hii ni sababu ya support kubwa niipatayo kutoka kwenu mashabiki zangu na kiukweli nimebarikiwa kuwapata nyie katika maisha yangu…my fans are so loyal sababu kila ninalowaomba bila pingamizi mmekuwa zaidi ya msaada kwangu katika kuhakikisha lolote nifanyalo hamniachi peke yangu bali mnaniunga mkono kwa njia moja au tofauti.Mara nyingi ninapokuwa katika kazi zangu napenda sana urembo wa macho sababu naweza sema imekuwa silaha au kitu pendwa zaidi kwa mashabiki zangu pale ninapokuwa katika uigizaji au katika maisha yangu nje ya sanaa,na katika kuhakikisha wakipendacho mashabiki zangu nakiboresha basi mara kwa mara nimekuwa nikiweka urembo wa kope ambao unafanya macho yangu kuwa kivutio zaidi either niwe na make up au bila make up mara zote nimekuwa nikiweka kope tokana na kazi au mazingira husika kwa wakati huo.Hivyo basi kwa sasa nimekuja na biadhaa yangu ninayoitangaza leo kwenu iitwayo I-Lashes by Irene Uwoya ambayo itapatikana Tanzania nzima katika maduka ya urembo yote yaliyo karibu nawe na kwa kuanza kwa wauzaji wa jumla punde nitaweka mawasiliano kwa ajili na kuweza kuweka order kulingana na uhitaji wako.Kwa mara nyingine Naombeni sana support yenu bila kunichoka na nina wapenda sana sana sana.I-Lashes ni kope ambazo unaweza tumia zaidi ya mara 3 na zenye uhalisia ufananao na kope zetu halisi kwa size na model tofauti tofauti,usikae mbali na page yangu ili upate update zaidi.
I’m not perfect but my lashes are…..

Well afromates what do you think ni move nzuri au lah?

Related posts

3 Comments

 1. boat car transport

  … [Trackback]

  […] Here you will find 29519 more Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/mapenzi-yake-na-kope-fake-yamemfanya-irene-uwoya-aje-na-bidhaa-ya-kope-fake/ […]

 2. 예능 다시보기

  … [Trackback]

  […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/mapenzi-yake-na-kope-fake-yamemfanya-irene-uwoya-aje-na-bidhaa-ya-kope-fake/ […]

 3. go to

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/mapenzi-yake-na-kope-fake-yamemfanya-irene-uwoya-aje-na-bidhaa-ya-kope-fake/ […]

Comments are closed.