Usafi wa mikono ni muhimu sana kwa binadamu, iwe mtu maarufu au wa kawaida, uwe wa kike au wa kiume wote tunatakiwa kuwa na mikono misafi, mikono misafi haichagui jinsia wala umri.
Katika pitapita zetu kwenye mitandao ya kijamii tumeona wasanii wetu wakijitahidi kuvaa vyema, na kutupa updates zao za mavazi pamoja na accessories hapa ndio tulipokuja kugundua wasanii wetu hawajui kuhusu usafi wa mikono mfano mzuri ni
Diamond Platnumz alipost picha yake hii akituambia tu-save tha date huku mikono yake ikonekana ameshikilia simu,ukiangalia huu mkono utagundua kwamba anang’ata sana kucha zake na hivyo zimepoteza ule mvuto. Japo si kawaida kwa mwanaume kukutwa na kucha ndefu lakini pia sio uzing’ate mpaka vidole vipoteze mvuto kata kucha zako na sugua vyema zikae katika hali ya usafi. Lakini pia inasemakana kung’ata kucha sio mazoea bali ni tatizo la kisaikolojia lakini pia unaweza kupata magonjwa kwa kula vijidudu/bakteria waliopo kwenye kucha

Mwingine ambae tulimuona ni Marioo, ukiangalia kucha za Marioo utagundua huyu si m-ng’ata kucha kabisa, kucha zipo kwenye shape nzuri hazijaharibika lakini tulichoona kwake ni kwamba hazisafishi. Ukiangalia vizuri hii picha utaona kucha katwa vyema, shape yake nzuri ila ndani ya kucha kuna uchafu, kukata kucha na kuziweka kwenye shape nzuri sio ndio mwisho wa kujali kucha zako hakikisha mara kwa mara unaondoa uchafu unaoingia kwenye kucha na wala haihitahi kuita mtu wa kukusafisha unaweza kufanya mwenyewe nyumbani na wala haichukui muda mrefu

Kuwa na kucha chafu au zisizokuwa katika hali nzuri sio tu zinakupa muonekano mbaya lakini pia unaweza kukosa wanawake, moja ya vitu ambavyo wanawake wanasema ni turn off kwao ni pamoja na mwanaume kutokujali mikono na kucha zake.
Unaweza kusoma hapa kuona namna unavyoweza kujali kucha zako hata nyumbani
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…