Matibabu ya uso kwa kutumia vitu vya jikoni kama kiini cha yai,machicha ya nazi,tango na limao.Treatment hii inaweza kufanyika Mara moja kwa wiki au kila baada ya wiki mbili, unaweza kufanya hata mara moja kwa mwezi ukipata nafasi kama unakuwa busy sana lkn matokeo mazuri utayashuhudia.
Namna ya kufanya
- Andaa maji masafi yenye joto kiasi unachomudu ktk ngozi yako, osha uso wako kwa hayo maji safi .
- Kama una ngozi kavu au ya kati chukua kipande cha tango kidogo na upake yale maji yake usoni,
- kwa wenye ngozi ya mafuta unaweza kutumia kipande cha limao kwa kupaka maji yake. Chukua pamba au kitambaa laini na futa maji ya matunda usoni kwa mtindo wa kusafisha taratibu usoni.
- Chukua machicha ya nazi na Anza kuusugua uso na shingoni taratibu Mpaka uridhike uso wote umepitiwa na machicha yako hasa unapoona unang’aa kwa mafuta kidogo yaliyotoka kwenye nazi. Kisha pukuta yale machicha ubaki na uso unaong’aa bila vitu vyeupe yaani machicha.
- Chukua kiini cha yai inapendeza ukitumia la kienyeji, au la kisasa lenye kiini cha njano iliyokolea angalau. Ili kiini kisijichanganye na ute wakati wa kupasua ,ligonge yai upande mmoja sio katikati na limimine ktk chombo mithili ya sahani ambayo unaona kiini katikati kisha unakichota na kuweka kando. Paka ule uji mzito wa njano wa kiini uso mzima bila kusahau shingoni na nyuma ya masikio na ngozi ya masikio.
- Baada ya kupaka kiini cha yai unaweza kuendelea na shughuli zako huku likiendelea kukauka,linapokauka ngozi yako inakuwa kama inajivuta vuta.
- Baada ya kule kuvuta kuisha inamaanisha yai limekauka kabisa. Osha uso wako kwa maji safi maji yawe ya baridi sasa.
Jinsi inavyofanya kazi
- Kuosha uso kwa maji yenye joto kunafungua matundu ya ngozi.
- Tango au limao hutumika kama cleanser, unapokuja kujifuta taratibu unaondoa uchafu katika ngozi yako.
- Machicha ya nazi yanatumika kama scrub, yanaondoa seli zilizokufa, kuifanya ngozi kuwa laini na kuipa mngao.
- Kiini cha yai hapa kinatumika kama maski, matundu ya ngozi yanajifunga vizuri na kinaipa ngozi yako lishe kutokana na vitamins zilizomo kwenye kiini cha yai kama vitamin E.
- Mwishoni unanawa na maji baridi ili kuruhusu matundu ya ngozi kujifunga na kuifanya ngozi ijiweke sawasawa.
Faida
- Husaidia kutibu na kuikinga ngozi na chunusi,
- Kuipa ngozi mng’ao bila kutumia kemikali za sumu,
- Husaidia kupunguza mikunjo ktk ngozi yako(wrinkles zinapungua)
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/matibabu-ya-uso-kwa-kutumia-vitu-vya-jikoni/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/matibabu-ya-uso-kwa-kutumia-vitu-vya-jikoni/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/urembo/matibabu-ya-uso-kwa-kutumia-vitu-vya-jikoni/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/matibabu-ya-uso-kwa-kutumia-vitu-vya-jikoni/ […]