Pamoja na kutumiwa kama kiungo katika mapishi mbalimbali. Chumvi ina umuhimu wake katika suala zima la urembo.
Je, unafahamu kuwa chumvi inaweza kutumika kama kipodozi na kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia?
Kumekuwepo na sababu mbalimbali zinazopelekea warembo kupata matatizo ya ngozi, kitendo hicho huwafanya warembo husika kupoteza nuru ya ngozi zao na pia matumaini ya kuonekana wenye kuvutia na kupendeza.
Matatizo ya chunusi, ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata mlundikano wa ngozi zilizokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kupelekea kutumia vipodozi visivyo salama kwa ngozi zao, kwa kutambua hilo wataalamu wa urembo wa asili walikuja na njia hii ambayo haina gharama kubwa ukilinganisha na njia zilizozoeleka na warembo wengi.
Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi wanalolifahamu hili, unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii machoni mara utakapoanza kuitumia.
Mahitaji.
- Chumvi ya unga kijiko 1 kikubwa
Namna ya kufanya
- Nawa uso wako kwa maji ya kawaida na kisha chukua kitambaa laini na safi. Chovya kwenye chumvi na kisha sugua katika ngozi yako ya uso taratibu.
- Baada ya kupaka katika uso mzima, weka chini kitambaa chako na kisha jisugue kwa kutumia mikono yako. Fanya hivyo hadi utakapoona takataka zinatoka.
- Baada ya kufanya hivyo kwa muda wa dakika mbili, osha kwa kutumia maji ya baridi.Ni muhimu kufanya zoezi hili mara kwa mara kwani bila hivyo krim au losheni “moisturizer” yako unayotumia haitafika katika ngozi pindi unapotaka kufanya hiyo.
- Unashauriwa kufanya aina hii ya scrub mara moja kwa wiki ili kupata matokeo mazuri.
Tahadhari : Matumizi ya chumvi kupitiliza sio mazuri utakuwa kwenye hatari ya kukausha mafuta ya asili ya Ngozi yako ambayo yanatakiwa kubaki ili kuilinda ngozi yako na mazingira! Tumia Kwa uangalifu!
©binturembo
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-chumvi-katika-urembo-wa-ngozi/ […]
… [Trackback]
[…] There you will find 64975 additional Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/matumizi-ya-chumvi-katika-urembo-wa-ngozi/ […]